Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Isdori Mpango, leo Jumapili tarehe 04 Septemba alifika msibani Chukwani Unguja kumpa pole Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefiwa na mwanawe Hassan hivi karibuni ambaye ni kaka wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi.
Post a Comment