Featured

    Featured Posts

MBUNGE MAHAWANGA AIBANA SERIKALI BUNGENI KUHUSU UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA MICHEZO KWA TIMU ZA WANAWAKE

Na CCM Blog

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Dar es Salaam Janeth Mahawanga ameihoji Serikali ieleze lini itawekeza katika Sekta ya Michezo hasa kwenye timu za Wanawake ili kuibua vipaji kwa watoto.


Mbunge Mahawanga ameihoji Serikali kueleza hayo, katika swali lake namba 112, alilouliza katika Kikao cha Bunge, Jijini Dodoma, leo.


"Je, ni lini Serikali itawekeza katika Sekta ya Michezo hasa kwenye timu za wanawake ili kuibua vipaji kwa watoto?" Aliuliza Mbunge Mahawanga.


Akitoa majibu ya swali hilo, kwa niaba ya Waziri wa Utamadunu, Sanaa na Michezo, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Pauline Gekul alisema:


"Mheshimiwa Spika, Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Elius Mahawanga (Viti Maalumu) kama ifuatavyo:-


Mheshimiwa Spika; Serikali imeendelea kuwekeza katika kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo ambapo kwa mwaka wa Fedha 2022/23 Shilingi Milioni 183.5 zimetengwa kama kianzio katika kutoa huduma kwa timu zetu za Taifa ikiwemo timu za wanawake na Shilingi Bilioni 10 zimetengwa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya michezo.


Aidha, Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika Timu za Taifa za wanawake ambapo kupitia uwekezaji huu timu hizi zimeendelea kufanya vizuri katika ukanda wa CECAFA na COSAFA na umewezesha timu ya Serengeti Girls kufuzu mashindano ya Kombe la Dunia nchini India.

Mbunge Janeth Mahawanga
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana