Featured

    Featured Posts

WCF YASISITIZA MAAFISA RASILIMALI WATU NA UTAWALA KUTUMIA TEHAMA KATIKA KUWASILISHA MADAI YA FIDIA KWA WAFANYAKAZI

Na K-VIS Blog/Khalfan Said, Morogoro
Maafisa Rasilimali Watu na Utawala hapa nchini wamehimizwa kutumia TEHAMA wakati wa kutoa Taarifa kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) pindi Mfanyakazi anapoumia, kuugua ama kufariki kutokana na kazi ili kuharakisha mchakato wa utoaji fidia.

Mwito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini wa Mfuko huo Dkt. Abdulsalaam Omar wakati akifungua Kikao Kazi cha Maafisa Rasilimali Watu na Utawala kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma kuhusu Huduma zitolewazo na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na umuhimu wa  kuzingatia Usalama na Afya Mahali pa Kazi, leo mjini Morogoro.

“WCF imetimiza miaka saba (7) tangu kuanzishwa kwake, katika kipindi chote hicho tumefanya maboresho mengi ya utoaji wa huduma, hivyo kuongeza elimu kwa wadau juu ya huduma zetu ni jukumu la msingi." Amesema

Alisema WCF inatambua dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi mahiri wa Mheshimiwa   Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri   ya   Muungano   wa Tanzania ni kuwa na uchumi endelevu na kuboresha hali ya maisha kwa wananchi wake kwa kutoa huduma bora.

“Dhamira hii itawezekana pale ambapo   tutakuwa na wafanyakazi wenye uhakika  wa afya zao kazini  na endapo   itatokea bahati mbaya wakapata madhara wakiwa  wanafanya  kazi basi wawe na uhakika wa kupata Fidia stahiki na kwa wakati na kwa kutumia TEHAMA hili linawezekana.” Alisema Dkt. Mduma.

Pamoja na matumizi ya TEHAMA Maafisa hao wamehimizwa kuambatisha nyaraka muhimu wakati wa kuwasilisha Madai.

Vile vile amesema  amesema matukio yanayotokea nje ya maeneo ya kazi mfano mfanyakazi anatoka nyumbani kwenda kazini au kazini kurejea nyumbani na au yuko katika safari ya kikazi na kwa bahati mbaya akapatwa na ajali lazima tukio hilo litolewe taarifa Polisi ambako atapatiwa PF3 kwa ajili ya matibabu na PF90 ambayo itaeleza jinsi ajali ilivyotokea na wahusika.

“Kwetu sisi nyaraka hizi ni muhimu sana, kwani ndizo zinathibitisha kuwepo kwa tukio na niwaombe ndugu washiriki, mfikishe ujumbe huu kwa wafanyakazi ili mchakato wa kulipa fidia uwe wa haraka.” Alibainisha Dkt. Mduma.

Akizungumzia ajali zinazotokea kwenye maeneo ya kazi  Afisa Mafao Mwandamizi wa WCF, Bw. Silvanus Kuloshe amesema  jicho la WCF ni Afisa Rasilimali Watu ambae atajaza fomu husika na kuziambatisha wakati wa kuwasilisha taarifa za Madai.

Kwa upande wao, washiriki wamesifu matumizi ya TEHAMA kwani yamekuwa yakirahisisha utoaji ya taarifa WCF pindi panapotokea matukio ya ajali au mfanyakazi akiugua.

“Mwanzo kulikuwa na changamoto wakati tukitumia mfumo wa kuwasilisha taarifa kwa dispatch…lakini mfumo huu wa WCF Portal umerahisisha uwasilishaji wa taarifa na hili ni jambo muhimu katika ulemwengu wa sasa.” Amesema Bw. Allan Gelege, mmoja wa washiriki

Naye Bi.Fatma Ramadhan, amesema amekuwa akitumia mifumo yote miwili, wa TEHAMA na ile ya kuwasilisha madai kwa dispatch,

Amesema Mfumo wa TEHAMA unatoa fursa ya kupata fomu zote zinazohitajika na hii imewarahisishia wanapohitaji kutoa taarifa pindi panapotokea tukio lolote na kumekuwepo na mawasiliano bora.

“Njia hii ni nzuri ukilinganisha na ile ya kutuma madaoii fisini kwa njia ya dispatch, ninawapongeza WCF kwa huduma hii kwani imekuwa rafiki katika mawasiliano baina yetu na wao.” Alifafanua Bi. Fatma ambaye yeye ni Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Dar es Salaam. 
Habari picha👇
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar (katikati) akifuatilia majadiliano ya vikundi vya Maafisa Rasilimali Watu.
Meneja Tathmini za Vihatarishi (WCF), Bi. Naanjela Msangi (kushoto), akielekeza jambo wakati wa majadiliano ya vikundi
Mkurugenzi wa Huduma za Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar (kulia) akifuatilia majadiliano ya vikundi.
Mmoja wa washiriki akichangia kwenye kikao kazi.
Mmoja wa washiriki akichangia kwenye kikao kazi
Majadiliano ya vikundi yakiendelea wakati wa kikao kazi
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada za kikao kazi.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada za kikao kazi.
Mmoja wa washiriki akichangia kwenye kikao kazi
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada za kikao kazi.
Afisa Mfawidhi WCF, Mkoa wa Morogoro, Bw. Athuman Khalfan (kushoto) na Afisa Tathmini Vihatarishi WCF, Bw. Robert Duguza (katikati) wakimsikiliza Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano WCF, Bi. Laura Kunenge mwanzoni mwa kikao kazi cha Maafisa Rasilimali Watu mjini Morogoro.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana