Afisa Mipango Miji ambaye pia ni Mratibu wa Urasimishaji Halmashauri ya Mji wa Makambako, Proin Safari akionesha orodha ya majina na gharama ya waliopimiwa viwanja vyao eneo la Sekondari-Maguvani Makambako mkoani Njombe, ambapo zaidi ya viwanja 1000 vilipimwa katika zoezi lililoendeshwa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) kwa kushirikiana na halmashauri hiyo.
MKURABITA Septemba 27, 2022 iliamua kufanya kampeni ya ufuatiliaji ili kujua utekelezaji wa mradi huo ambao umegharibu zaidi ya sh. milioni 75 zilizotolewa na serikali kupitia MKURABITA. Ufuatiliaji huo uliongozwa na Meneja Urasimiashaji mijini wa mpango huo ambaye pia alikuwa kiongozi wa upimaji wa eneo hilo, Mwesiga Ileta.
Mkazi wa Mtaa wa Sekondari ambaye amepata hatimiliki baada ya viwanja vyake kupimiwa na MKURABITA akielezea jinsi atakvyonufaika.Mwenyekiti wa Mtaa wa Sekondari , Kata ya Maguvani Makambako, Nsangalufu Mwakasumbula ambaye kwa niaba ya wananchi wa eneo hilo, ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuiwezesha MKURABITA kufanikisha upimaji viwanja katika eneo hilo.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Meneja Urasimishaji Mijini wa MKURABITA, Mwesiga, Afisa Mipango Miji wa Makambako, Safari na wananchi wa eneo hilo wakielezea utekelezaji na manufaa ya mradi huo...
Post a Comment