Askofu Mstaafu wa Kanisa Katoliki,Jacob Koda ameiomba Serikali kufufua Viwanda vyote vilivyokuwa vikifanya uzalishaji enzi za Mwalimu Nyerere ikiwa kama njia mojawapo ya kumuenzi Mwalimu.
Askofu Koda aliyasema hayo wakati akitoa mada kuhusu Mchango wa Mwalimu katika kukuza uchumi na Maendeleo endelevu ambapo alisema Nyerere alijitahidi kuanzisha viwanda katika mikoa mbalimbali ili kukuza uchumi.
Alisema Baba wa Taifa alitambua ili nchi iweze kuwa na Maendeleo endelevu lazima kuwe na viwanda na ndipo alipoanzisha viwanda vya nguo kwenye mikoa karibu yote,kulikuwepo na viwanda vya ngozi vikitengeneza viatu,mabegi,kulikuwepo na viwanda vya magunia na kiwanda Cha General Tyre cha Arusha ambacho kilikuwa kinaaaminika kwa matairi bora Afrika Mashariki.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye alikua mgeni rasmi katika Kongamano hilo aliahidi kuuchukua ushauri huo wa Askofu na kuufanyia kazi.
Post a Comment