Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema anatamani watanzania wote kuunga mkono Bima ya Afya kwa Wote inayotarajiwa kuanza siku za usoni baada ya muswada kupitishwa bungeni na Rais kusaini ili iwe sheria kamili.
Aidha, ameviomba vyombo vya habari nchini kuisemea vizuri n Bima ya Afya kwa Wote.
Amebainisha hilo alipokuwa akihitimisha mkutano kati ya Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), Mavere Tukai na vyombo vya habari kwenye Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO jijini Dodoma Oktoba 17, 2022.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Msigwa akielezea umuhimu wa bima hiyo...
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM
0754264203
Post a Comment