WAZIRI MKUU ATEMBELEA ENEO YANAPOJENGWA MABEHEWA YA TRENI YA SGR
*Ni yale yanayotengenezwa nchini Korea Kusini kwa ajili ya SGR
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maendeleo na kasi ya ujenzi wa mabehewa mapya kwa ajili Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania unaofanywa na Kampuni ya Sung Shin Rolling Stock (SSRT) iliyoko nchini Korea Kusini.
“Kati ya mabehewa 81 ambayo Tanzania inatengeneza kutoka kwenu, tayari 36 yamekamilika na yameshapelekwa nchini Tanzania na 45 yaliyobaki yanategemewa kukamilika Machi, 2023. Mabehewa haya ni ya daraja la tatu na yatatoa huduma zote muhimu.” amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Oktoba 25, 2022) mara baada ya kutembelea kampuni ya SSRST inayotengeneza mabehewa na injini za treni nchini Korea Kusini.
Kadhalika, Waziri Mkuu amemkaribisha nchini Rais wa Kampuni hiyo Gye Shul Park aje kuwekeza nchini Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo mpango wa Serikali wa kuendelea kuiboresha sekta ya usafiri wa reli
“Mnakiwanda kikubwa, teknolojia ya hali ya juu pamoja na utaalamu na watalaam kwenye eneo hili. Kwa sasa tuna mipango mikubwa ya kuendelea kuiboresha sekta hii ya usafiri wa reli, yapo maeneo tofauti kwenye mpango wa kuunganishwa na reli ya kisasa (SGR), nakukaribisha kuja kuwekeza kitu kama hiki Tanzania.”
Wakati huohuo, Waziri Mkuu ametembelea Kituo cha Seamul Undong ambacho ni taswira ya maendeleo ya Korea kupitia mpango wa kuviwezesha vijiji ambao unatekeleza mpango huo nchini Tanzania katika mkoa wa Morogoro (Pangawe) na Zanzibar.
Waziri Mkuu amemshukuru Rais wa Kituo hicho na kumuomba kuendelea kutoa ushirikiano ili kukuza zaidi mpango huo na kufikia maeneo mengi zaidi.
“Mfumo huu kwasasa umekuwa wa kitaifa, ushirikishwaji wa Wananchi ni mkubwa, sasa tunataka tuikuze zaidi, haya maeneo ya Morogoro na Zanzibar tunataka yawe mifano, kwenye utekelezaji wa eneo hili”, akasema Waziri Mkuu.
Pia, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kituo cha Ubunifu cha CEIC kilichopo katika mji wa Pangyo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Bw. Gye Shul Park ambaye ni Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sung Shin Rolling Stock ya Korea (kushoto kwake) kuhusu mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) wakati alipotembelea karakana ya kutengeneza mabehewa ya treni inayomilikiwa na kampuni hiyo, Oktoba 25, 2022. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja ya mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo yanatengenezwa katika kiwanda cha kampuni ya Sung Shin Rolling ya Korea. alipotembelea kiwanda hicho leo Oktoba 25, 2022. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Korea, Balozi ogolani Mvura, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mabarouk, Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni yaSung Shin Roliing, Gye Shul Park na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja ya mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo yanatengenezwa katika kiwanda cha kampuni ya Sung Shin Rolling ya Korea, kiwa katika ziara ya kikazi nchini humo leo. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Korea, Balozi Togolani Mvura, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mabarouk, Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Sung Shin Roliing, Gye Shul Park na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Chini ni picha Waziri Mkuu Majaliwa akiwa katika matukio mbalimbali nchini Korea Kusini👇
Post a Comment