Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ameagiza Kampuni zote za Mawasiliano ya Simu Nchini kuanzisha huduma maalumu kwa ajili ya Vikundi vya Wajasiriamali Wadogo Wanawake ili viweze kufanya kwa urahisi na kwa gharama nafuu Biashara kwa njia ya Kidigitali.
Katika kuhakikisha agizo hilo linatekelezwa Waziri Nape ametoa siku 14 kuanzia leo Oktoba 8, 2022 Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) kukutana na Kampuni hizo za utoaji wa Huduma za Mawasilino ili kuweka mfumo huo na kuagiza kwamba mbali na kuuweka, lakini pia uwe wa gharama nafuu.
Waziri Nape ametoa agizo hilo leo, wakati akihutubia baada ya kufungua Maonyesho ya Kongamano 'Women Of Hpe Alive (WHA) la Wanawake Wajasiriamali, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, ambalo limehudhiriwa na wanawake zaidi ya 6000 kutoka Vikundi mbalimbali vya Wanawake Wajasiriamali wadogo na wakati vilivyopo chini ya usaidizi wa WHA.
Waziri Nape ametoa agizo hilo, akijibu moja ya maombi yaliyotajwa na WHA katika risala iliyosomwa kwake na Katibu wa WHA Saumu Mbwana, wakati wa hafla hiyo ambapo aliomba Kampuni Mawasiliano ya simu kupitia TCRA ziweke huduma rafiki itakayowawesha Wajasiliamali Wadogo na Wakati Wanawake kuweza kufanya mawasiliano ya biashara kidigitali kwa urahisi na bei nafuu.
"Zipo huduma za Wapenzi, Michezo nakadhalika zinazotolewa na Kampuni za Simu, sasa mimi sioni kama kuna ugumu wowote kwa kampuni hizi kuanzisha huduma hii kwa Wanawake Wajasiriamali wa WHA, ili muweze kufanya shughuli zetu za kibiashara kidigitali kama mlivyodhamiria.
Hivyo kwa kuwa jambo hili linawezekana, naiagiza TCRA kukutana na Kampuni hizi zote za simu ndani ya siku 14 ili kuweka huduma hii mara moja", Akasema na kuagiza Waziri Nape.
Waziri Nape aliwapongeza WHA kwa kuja na wazo la kuingia katika Uchumi wa Kidigitali, akisema ni wazo zuri sana kwa kuwa wamekuja nalo katika wakati muafaka, kwa sababu ndivyo dunia sasa inavyotaka maaba imefikia wakati ambapo inawezekana kufanya biashara kwa njia ya mtandao.
Alimpongeza Mwanzilishi wa WHA, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Dar es Salaam Janeth Mahawanga kwa kuja na kufanikisha wazo wa kuwakusanya Wanawake Wajasiliamali hasa wa mkoa wa Dar es Salaam, kwa kuwa hilo siyo jambo rahisi hasa wa mtu ambaye ni mara ya kwanza kuwa Mbunge.
"Mimi najaua ikiwa ndiyo mara ya kwanza mtu kuwa Mbunge wengi huhangaika kwanza kutafuta apitie wapi ili kuja na wazo lenye tija na likafanikiwa. Hili alilofanya ni jambo kubwa sana kwake, kwa maana nyingine ni sawa na mtoti aliyezaliwa akiwa mkubwa", akasema Nape.
Mapema akifungua Kongamano hilo, Mbunge Janeth Mahawanga alisema, alisema ni Kongamano la nne kufanyika tangu WHA ilipoanzishwa mwaka 2012 na katika jitihada za kulibiresha safari hii wameamua liambatane na maonyesho ya bidhaa na huduma mbalimbali za Wanawake, ili Wanawake hao chini ya WHA wapate fursa za kutangaza na kuuza bidhaa na huduma hizo.
Mbunge Mahawanga aliwataka wanawake kupitua WHA sasa 'kukomaa' zaidi kama moja ya njia ya kuuga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani katika kuwainua kimaisha Kina Mama wote hapa nchini, kwa kuwa tofauti na mwanzo ambapo kikwazo kikubwa ilikuwa mikopo, sasa kikwazo hizo hakipo.
" Wakati tunaanzisha harakati hizi za kuwainua Kinamama, kulikuwa na changamoto cha upatikanaji motaji, Rais wetu Samia amepambana na sasa mikopo kwa Wanawake hasa ile inayotolewa kupitia Halmashauri kote nchini inapatikana, hivyo ndugu zangu Wanawake, ni lazima tuchangamke ili kumuunga mkono Rais wetu", akasema Mbunge Mahawanga.
Mapema katika Katibu Saumu alisema, "Sisi ni kikundi cha Kikoba cha kinamama120 ambao tunatoka Kata tofauti tofauti ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, tukiwa tumechanganyika kutoka taaluma mbalimbali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi lakini pia kuhakikisha wenzetu wa Mkoa wa Dar es Saalaam wananufaika na uwepo wa kikundi chetu.
Kikundi chetu kilianza mwaka 2012 na mpaka sasa miaka kumi tukiwa tumeshikana kwa kudumisha amani, upendo na ushirikiano wa hali ya juu sana ambao umetupelekea kupata tuzo ya heshima na kuwa Kikundi bora cha Kikoba kwa mwaka 2021.
Kwa mwaka huu wa 2022 tumefanikiwa kuanzisha vikundi Vidogo vitatu vilivyo chini ya Mwamvuli wa WHA kila kikundi kina wanachama wasiopungua 30. Lengo la kuanzisha vikundi hivi ni kuwashika Mkono wamama wenzetu ili nao waweze kuinuka kifikra na kiuchumi; kwani kujiunga kwao kutapelekea kupata mikopo midogo midogo na yenye riba nafuu.
Sisi kama wanawake na kuhakikisha tunaenda kidijitali kama kauli mbiu yetu inavyojieleza tumefanikiwa kuwekeza Sh. 112,000,000. katika mfuko wa UTT, Fedha hizo zinajizalisha na kwa mwaka tunaweza kupata faida si chini ya fedha sh. 12,000,000.
Vilevile hadi sasa kikundi chetu kina mtaji wa Sh. Milioni 600 ambazo tumeweza kuweka kwenye Microfinance yetu (WHA Microfinance) iliyozinduliwa rasmi mwaka 2021na kwenye biashara ndogondogo za kikundi chetu.
Picha za matukio ya Hafla hiyo mwanzoni👇
Washiriki wakijisajili kuingia ukumbini
Katibu wa WHA Saumu Mbwana (mwenye Bahasha ya kaki) akienda kusoma risala |
Katibu wa WHA Saumu Mbwana akisoma risala |
Katibu wa WHA Saumu Mbwana akikabidhi risala kwa Waziri Nape. |
Mwenyekiti wa WHA Janeth Mahawanga akimkaribisha Waziri Nape kufanya uzinduzi wa Kongamano hilo na kuhutubia |
Mwenyekiti wa WHA Janeth Mahawanga akimkaribisha Waziri Nape kweye eneo la kuhtubia |
Waziri Nape akihutubia kufungua Kongamano hilo
Washiriki wakimsikiliza waziri Nape
Washiriki wakimsikiliza Waziri Nape
Nashiriki wakimsikiliza Waziri Nape
Wageni Waalikwa wakimsikiliza Waziri Nape
Waziri Nape akongozana na Mwenyekiti Mahawanga kwenda kuzindua rasmi Kongamano hilo.
Waziri Nape akikata utepe kuzindua Kongamano hilo.
Waziri Nape na Mwenyekiti Mahawnaga wakishangilia baada ya kuzindua kongamano hilo
Mwenyekiti Mahawanga akizungunza baada ya Waziri Nape kufanya uzinduzi huo.
Waziri Nape akimtuza msanii aliyekuwa akitumbuiza wakati wa uzinduzi huo. Halafu zikafuatia picha za pamoja Waziri na Mwenyekiti Mahawanga na Makundi mbalimbali👇
Mwenyekiti Mawanga akiteta jamboi na Waziri Nape. Kisha picha za makundi zikaendelea
Mwenyekiti wa WHA Mbunge Mahawanga akimkabidhi tuzo Waziri Nape kwa kuhudhuria hafla hiyo.
"Sasa kabla sijashuka hapa jukwaani, naomba niwaambie jambo lingine muhimu; Kwa bahati nzuri mmepata kiongozi Rais Samia ambaye ni mwanamke mwenzenu, sasa nawaomba mumuunge mkono kwa dhati, maana amejitahidi kwa mafanikio makubwa kufanya mambio mengi kiasi kwamba saa Tanzania inag'ara Kimataifa. Muombeeni aendeletee kulitumikia Taifa letu kwa amani, utulivu", akasema Nape.
Wziri Nape akitoka jukwaani baada ya kuhutubia.
Kisha akakata keki ya miaka kumi ya WHA
Akamlisha kipande Mwenyekiti Mbunge Mahawanga.
Haklafu akamlisha Katibu wa WHA.
Haklafu akasindikizwa na Mwenyekiti wa WHA Mbunge Mahawanga kutoka ukumbini.
Waziri Nape akaagana na wadau wakati wakitoka.Waziri Nape akaagana na Mwenyekiti Mbunge Mahawanga na viongozi wengine wakati akiongoka.
©Oct 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
Post a Comment