Benki ya NMB mkoani hapa imetoa msaada wa madawati, viti na meza kwa shule tatu za msingi na mbili za sekondari zilizopo katika Halamshauri ya mji wa Nanyamba vyenye thamani ya Sh22 million.
Msaada huo ulikabidhiwa na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini, Janeth Shango kwa mkuu wa wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya jana katika shule ya Msingi Dinyecha.
Madawati hayo yatagaiwa kwa shule za msingi tatu za Kiwengulo, Mibobo na Dinyecha na shule za sekondari za Mnima na Nitekela zote za halmashauri ya Mji wa Nanyamba.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Mwalimu mkuu wa shule ya Dinyecha, Shafii Abdallah Moto ambaye shule yake imepata madawati 50, alisema kuwa msaada huo utamaliza changamoto ya madawati miongoni mwa wanafunzi wake wa kawaida ambao mahitaji kwa ujumla ni madawati 205 kwa wanafunzi 594. Shule hii pia ina kitengo cha watoto wenye ulemavu wa akili.
“Madawati hamsini yataondoa kabisa tatizo la vifaa hivyo shuleni kwetu na hii itawafanya wanafunzi kujielekeza katika masomo yao” alisema Moto.
Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Dunstan Kyobya alisema kuwa halmashauri ya Nanyamba ina shule za msingi 67, mahitaji ya madawati 8167 lakini yaliyopo ni 7121 kwa hiyo kuna upungufu wa madawati 1044.
“Msaada huu mlioutoa unaenda kupunguza kero tuliyonayo ya upungufu wa madawati katika Halmashauri hii” alisema Kyobya.
Kyobya alisema Halmashauri hiyo ina mahitaji ya viti na meza 4687 katika shule zake za sekondari 12, upungufu wa viti 150 na meza 150 kwa hiyo msaada wa NMB umepunguza mapungufu hayo.
Shango alisema kuwa benki hiyo inawajibika kushirikiana na jamii kutatua changamoto ambazo zinawakabili wanajamii ikiwemo za sekta ya elimu, afya na majanga.
Alisema katika elimu benki hiyo inaamini kwua ndio litapatikana taifa lililo bora na makini.
“Naipongeza serikali ya awamu ya sita ya Samia Suluhu Hassan kwa kuleta amendeleo bora kwa waoto kysoma vzuri na sisi kama wadau tunao wajibu wa kushirikiana na serikali ndio maana tumefika hapa leo” alsiema Shango.
Mwanafunzi wa darasa la sita, Yumna Ramadhani ameishukuru benki ya NMB kwa msaada wa madawati na kueleza kuwa sasa watakaa kwa utulvu na kuandika vizuri tofauti na mwanzo.
Post a Comment