Kigamboni, Dar es Salaam
Balozi wa Mazingira nchini Mwanadada Winfrida Shonde ambaye alichaguliwa hivi karibuni kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Kigamboni jijini Dar es Salaam, ameendelea kuonyesha kuwa chachu kwa kujituma katika kuijenga CCM na kujitolea kwa taifa katika masuala ya maendeleo.
Katika jitihada zake hizo, hivi karibuni mpambanaji huyo kijana kabisa Winfrida Shonde alitoa mchango wa matofali elfu moja (1000) kwa ajili ya kusaidia ujenzi nyumba ya Katibu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam.
Baada ya kutoa mchango huo baadaye Winfrida Shonde kupitia ukurasa wake wa @winnies_hints
aliwahamaisha wanachama wenginena wa CCM hasa vijana kujituma kwa hali na mali kusaidia juhudi za Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Samia katika kukiimarisha Chama na kuiletea Maendeleo Tanzania.
“Tuendelee kufanya kazi kwa juhudi na maarifa, huku tukisapoti juhudi za Mama @samia_suluhu_hassan kwa vitendo. kujitolea kwangu huku ndani ya CCM sio kwamba ninao uwezo zaidi, bali napenda kuwa sehemu ya mafanikio na jitihada zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mwenyekiti wa CCM rais Samia Suluhu Hassan.
Nafanya hivi pia kama mzalendo wa nchi yangu na Mjumbe wa Halmashauri kuu Wilaya Kigamboni, niwajibu wangu kujitolea kwa maslahi mapana ya Taifa hili na watu wake, hili liwe chachu kwetu sote kuwa ni jukumu letu sote hasa vijana kuijenga Tanzania tuitakayo.” akaandika Winfrida Shonde katika ukurasa wake huo.
Post a Comment