Na Bashir Nkoromo, Dar es Salaam
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali Dk. Boniphace Christopher Luhende kuwa Wakili Mkuu wa Serikali kuchukua nafasi ya Gabriel Paschal Malata aliyeteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu jijini Dar es Salaam, Oktoba 10, 2022, imesema Rais amemteua pia aliyekuwa Wakili wa Serikali Mkuu katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Sarah Duncan Mwaipopo kuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Luhende ambaye ametuliwa kuwa Wakili Mkuu wa Serikali.
Taarifa imesema Uteuzi huu umeanza juzi tarehe 09 Oktoba, 2022.
Rais Samia Suluhu Hassan kazini.
Post a Comment