Na Lissa Mbozi, Songwe
Wakati Maonyesho ya mbolea Duniani yanaanza leo Oktoba 1, 2022, Kampuni ya SBL inayozalisha mbolea ya GPC kutoka Kenya imeahidi kugawa bure mifuko 2,500 ya mbolea hiyo kwa wakulima watakaofika kwenye Viwanja vya Kimondo Mloo Mbozi mkoani Songwe ambako ambako Maonyesho hayo yanaanza leo Kitaifa.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo ya SBL Joe Kairuki amesema Kampuni hiyo inatarajia kugawa bure mifuko hiyo 2,500 ya mbolea kwa wakulima watakao fika kwenye Maonyesho hayo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuwainua wakulima nchini.
Amesema, GPC imefanya vizuri nchini Kenya na anaamini italeta tija kubwa kwa wakulima hapa Tanzania na kuwasihi wakulima kujitokeza kwa wingi kuchukua mbolea hiyo bure katika siku 3 za maonyesho hayo.
Post a Comment