Moshi, Kilimanjaro
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro umesema hautamvumilia kijana yoyote atakayebeza maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan
Hayo yamesemwa mjini Moshi na Mwenyekiti wa Umoja huo, Yuvenal Shirima wakati akiongea na waandishi wa habari na kuongeza kuwa iko haja kwa serikali kuwachukulia hatua kwa wale wote wanaokebehi Maendeleo yaliyopo ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na barabara ambazo zimejengwa katika awamu hii.
Shirima amesema Mheshimiwa Rais Samia amefanya kazi ya kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa watanzania na kwamba wao kama vijana hawako tayari kuona mambo mazuri yaliyofanywa na Rais yakiligawa Taifa kwa propaganda za mitandaoni.
“ Nichukue nafasi hii kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiongoza nchi yetu kwa umahiri mkubwa na kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano kwa watanzania katika kipindi chote tangu aingie madarakani” alisema Shirima.
Oktoba 3 mwaka huu kulisambaa kipande cha video kikimnukuu Spika wa Bunge dokta Tulia Akson akizungumza na vijana wa hamasa ambapo aliwaeleza kushughulika na watu watakaobainika kumsema vibaya yeye na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya Vyama vya Upinzani walitumia nafasi hiyo kumkashifu Mheshimiwa Rais Samia pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Tulia Akson jambo limepingwa vikali na Umoja wa Vijana wa CCM moshi vijijini.
Post a Comment