Na Mwandishi Maalum, Pwani
Uongozi wa Shule ya Sekondari Ruvu katika mkoa wa Pwani umesema kiasi cha zinahitajika kiasi cha Sh. milioni 794.9 kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa uzio kwenye shule hiyo kwa lengo la kuimarisha usalama wa wanafunzi 850 wa kike wanaosoma katika shule hiyo.
Akizungumza jana wakati wa tukio la upokeaji wa vifaa vya ujenzi (matofali na nondo) vilivyotolewa na wanafunzi waliosoma shule hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 1977 mpaka sasa, Mkuu wa Shule ya Ruvu Sekondari Juliana Chimanzi alisema uzio wa shule ni muhimu kwani kuna changamoto ya mifugo kuingia eneo la shule lakini pia wezi na vibaka.
"Nitoe Serikali, wadau na kwa namna ya kipekee wanafunzi waliopita hapa kokote waliko watusaidie.Shule yetu ina idadi kubwa wanafunzi wasichana ambao wanafikia 850 , tunahitaji kuweka ulinzi kwa kujengewa uzio.Tumefanya tathimini Sh.Sh.milioni 794.9 zinahitajika,”aamesema.
Awali akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo vya ujenzi, Mwenyekiti wa Wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo kwa nyakati tofauti Veronica Chambuso kuanzia mwaka 1977 amesema wameona wachangishane ili peleka vifaa vitakavyosaidia kuanza ujenzi wa uzio.
“Tumeleta matofali na nondo , huu ni mwanzo lakini tunaendelea kuwaomba waliosoma Ruvu Sekondari kuanzia mwaka 1977 mpaka sasa na miaka inayokuja, wazazi , wafadhili na wale wanaoguswa na ulinzi wa watoto wa kike tushirikiane kwani ukimlinda mtoto wa kikekwani akapata elimu itamsaidia na taifa litanufaika,”alisema Chambuso.
Amefafanua kwamba shule hiyo ilijengwa mwaka 1977 baada ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuomba msaada Serikali ya Cuba, hivyo wanamshukuru kwa upendo wake na katika kumuenzi wameona kuna uhitaji mkubwa wa uzio.
Kwa upande wao Waratibu wa Uchangiaji huo ambao nao ni sehemu ya wanafunzi waliosoma shule hiyo Devota Makililo na Victoris Massawe wameendelea kuhamasisha wadau kuendelea kuchangia ujenzi huo.
“Tunaomba wadau na Wizara ya Elimu kuona huruma kwa shule ya wasichana watusaidie kwenye kujenge uzio.Pia kwa unyenyekevu mkubwa tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan atusaidie kufanikisha ujenzi huu.Watoto kike wakihitaji kuangaliwa na amekuwa akilisemea hilo mara kwa mara,”ameongeza.
Wakati huo huo Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruvu Jacquline Mgisha anayesoma kidato cha Sita alisema wanashukuru wanafunzi waliopita shuleni hapo kutambua umuhimu wa jambo hilo.
“Uzio ni muhimu sana kwetu , hivi makazi ya watu yamekuwa karibu na shule na hivyo kuhatarisha usalama wa wanafunzi.Pia tunamuomba mama yetu Rais Samia Samia Suluhu kutusaidia na hatimaye tuwe na uzio na sisi tutamlipa kwa kufanya vizuri kwenye masomo,”amesema.
Victoris Massawe (Wapili kulia) ambaye ni moja ya wanafunzi waliosoma katika Shule ya Sekondari Ruvu ambaye pia ni mmoja ya Waratibu wa michango ya wanafunzi akikabidhi tofali kwa Waziri Mkuu wa Wanafunzi wa Shule hiyo Minael Katamba (kushoto) jana baada ya wanafunzi waliosoma kwenye shule hiyo kuanzia mwaka 1977 mpaka sasa kuamua kuchangia vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa uzio wa Shule hiyo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ruvu mkoani Pwani wakiwa wamebeba keki iliyotolewa na wanafunzi waliosoma katika shule hiyo kuanzia mwaka 1977 hadi sasa ikiwa ni ishara ya kuzindua Kampeni ya ujenzi wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kujenga uzio wa Shule hiyo ili kuimarisha usalama wa wanafunzi wa kike.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Ruvu mkoani Pwani Juliana Chimanzi (wa tatu kulia) akiwa na baadhi ya walimu waliofundisha katika shule hiyo( walioko kulia) wakiwa na baadhi ya wanafunzi waliosoma shuleni hapo kuanzia mwaka 1977 wakikata keki kuashiria uzinduzi wa Ujenzi wa uzio wa Shule hiyo .Wanafunzi hao wameamua kuchangishana fedha ili kusaidia kununua sehemu ya vifaa vya ujenzi na kukabidhi kwa uongozi wa Shule hiyo jana
Wanafunzi wa kwanza kabisa kuanza kusoma katika Shule ya Sekondari Ruvu iliyoanza mwaka 1977 wakijitambulisha kwa wanafunzi na walimu walioko sasa baada ya kufika shuleni hapo kwenye tukio la kukabidhi vifaa vya ujenzi nondo na matofali ili kuanza ujenzi wa uzio wa Shule hiyo.
Post a Comment