Wageni hao (kushoto) na Wenyeji wao ambao ni Watekeleza Sauti wa Kanisa Halisi wa Kao Kuu na wa vituo vya mikoani na nje ya Nchi (kulia) wakiendelea kuimba nyimbo za shangwe nje ya ukumbi wa Kanisa hilo. Kaka Huduma akicharaza kinanda wakati wanamuziki wa nyimbo za kumwinua Chanzo Halisi walipokuwa wakipiga wimbo wa kuwapokea wageni hao Waimbaji wa nyimbo za kumtukuza Chanzo Halisi wakiimba wimbo wa kuwapokea wageni hao. Wageni hao kutoka mkoani Njombe wakaanza kuingia katika ukumbi wa Kanisa. Baba Halisi akiwatazama kwa furaha wageni hao kutoka Njombe walipokuwa wakiingia ukumbini.
Baada ya wageni kuingia ukumbini Baba na Mama Halisi wakawapokea. "Nimefurahi kuwana, imekuwa Baraza sana kwetu kuja kututembelea, sasa najua mmekuwa na safari ndefu, tumewaandalia chakula cha jioni, kwa hiyo mle kwanzahalafu tuongee kidogo kisha mkapumzike tulikowaandalia", akasema Baba Halisi kuwakaribisha chakula wageni wake. Baada ya kuwakaribisha Chakula Baba Halisi na Mama Halisi wakaketi na wageni pia wakiwa wameketi kabla ya kusimama kwenda 'kujisevia' chakula. Kisha wageni wakiwa na wenyeji wakaanza kupata 'starter' ya kukaribisha mlo wenyewe👇
===========
Kisha Wakaanza kupata mlo wenyewe wakiongozwa na Mtekeleza Sauti Mwenyeji 👇
Baba na Mama Halisi 'Wakiwasindikiza' wageni kushiriki Matunda (chakula).👇 Uzao na Watekeleza sauti nao wakashiriki matunda👇 ==============Baada ya Chakula Baba Halisi akawashukuru wageni wake na kufanya shukurani kwa Chanzo Halisi na kuwaruhusu kwenda kupumzika👇
Baba Halisi akifanya Shukurani👇 ==================== Baada ya kufanaya shukrani Baba Halaisi akiondoka kwenda kupunzika mwishoni hafla hiyo.©Nov. 2022 CCM Blog/Bashir Nkoromo
Post a Comment