Dkt Bashiru Ali Kakurwa
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umemjia juu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt Bashiru Ali Kakurwa kwa kauli zake zisizofaa za kuwachonganisha viongozi na wananchi, ikiwemo aliyoitoa akihutumia mkutano wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA) mjini Morogoro kwamba viongozi hawapaswi kusifiwa kuwa wanaupiga mwingi wanapotekeleza majukumu, hivyo kumtaka ajitathmini na kuomba radhi.
Karipio hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa, Kenan Kihongosi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari katika Makao Makuu ya umoja huo jijini Dodoma Novemba 19, 2022.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Kihongosi akitoa karipio hilo....
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment