Featured

    Featured Posts

CCM YAWASHUKURU WATANZANIA KWA UENDELEA KUIAMINI NA KUIPATIA USHINDI WA KISHINDO UCHAGUZI MDOGO ULIOFANYIKA JUZI

CCM Blog, Dar es Salaam
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetoa Shukrani kwa Watanzania kuendelea kukiamini na hivyo kukipatia ushindi wa kishindo katika Uchaguzi mdogo uliofanyika juzi, Disemba 17, 2022 kujaza nafasi iliyokuwa wazi ya Ubunge Jimbo la Amani wilaya ya Mjini mkoa wa Mjini Mgharibi Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka pia inatoa Shukrani hizo kwa Watanzania kuiamini na kuwezesha kupata ushindi wa kishindo katika Uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika katika jumla ya Kata 7 kati ya 12. 

Shaka amezijata Kata hizo kuwa ni Majohe (Dar es Salaam), Mwamalili (Shinyanga), Njombe (Njombe), Vibaoni na Mnyanjani (Tanga),Mndumbwe (Mtwara), Dunda (Pwani) na Kata 5 kati ya 12 ambazo tayari CCM ilishinda kwa kupita bila kupingwa na kuzitaja Kata hizo kuwa ni Dabalo (Dodoma), Ibanda (Mbeya), Misugusugu (Pwani) Kalumbeleza (Rukwa) na Lukozi (Tanga).

"Siri ya Ushindi huu wa CCM ni umoja na mshikamano ulipo ndani ya Chama, Uteuzi wa wgombea bora, kampeni za kisasa zilizowafikia wapigakura, uadilifu na uaminifu katika kuwatumikia wananchi hususani katika kukidhi mahitaji na matarajio yao katika kuwaletea maendeleo", amesema Shaka. Tafadhali isome taarifa kamili kama iliyotolewa na Shaka, hiyo Hapo👇











author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana