Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Aloyce Mwogofi akielezea umuhimu wa anuani za makazi kwa wafanyabiashara alipokuwa akifungua mafunzo kwa wanayabiashara yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasliano na Teknolojia ya Habari jijini Dodoma Disemba 13, 2022.
Mjumbe wa Timu ya Uratibu Mfumo wa Anuani za Makazi Kitaifa, Arnold Mkude akielezea muundo wa mfumo wa anuani za makazi na manufaa yake.
Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano Wizara ya Habari, Mawasliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza akisema neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.
Mtaalamu wa Mfumo wa Kidijitali wa Anuani za Makazi, Masele Mabula akielezea kuhusu postikodi
Baadhi ya maafisa wa serikali.
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa katika mafunzo hayo
Baadhi ya Wanahabari wakiwa katika kikao hicho
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeeleza kuwa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi nchini, unawezesha mipango na tafiti kufanyika kwa tija, kuongeza vyanzo vya fedha, kuimarisha usalama ,kuwezesha utoaji , upatikanaji na upelekaji wa huduma za bidhaa hadi mahali husika.
Hayo yamebainishwa na Mjumbe wa Timu ya Uratibu Mfumo wa Anwani za Makazi Kitaifa, Arnold Mkude kwenye kikao kazi kati ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari na wafanyabiasha wa Jiji la Dodoma kuhusu umuhimu wa utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi.
Ametaja manufaa mengine kuwa ni kusaidia wawekezaji kufanya uamuzi kabla ya kufanya uwekezaji na kuwezesha biashara mtandao kufanikiwa hali itakayo inua fursa ya uchumi wa kidigitali.
Pamoja na hayo alitumia nafasi hiyo kueleza muundo wa anwani za makazi kwa upande wa vijijini kuwa unahusisha namba ya nyumba au jengo, jina la kitongoji au shehia na namba maalumu ya postikodi na kwa upande wa Miji, muundo wa anwani za makazi unahusisha namba ya nyumba ,jina la mtaa au barabara,namba ya kata au postikodi.
"Jamii inapaswa kutambua kuwa postikodi ni utaratibu wa kitaalam unaotumika kutenga maeneo ya makazi wakati amwani za makazi ni miundombinu ambayo kwa pamoja inatambulisha mahali halisi mtu ama kitu kilipo, aina hii ya utambulisho inaundwa na vitu vikuu vitatu ambavyo ni namba ya anwani, jina la barabara na postikodi,"alifafanua
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Aloyce Mwogofi amesema kikao kazi hicho ni muhimu kwa kuwa kinalenga kujenga uelewa wa pamoja katika kuhamasisha matumizi ya anwani za makazi na kueleza kuwa wananchi hususani wafanyabiashara wanapaswa kutumia mfumo wa anwani za makazi.
Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria mafunzo hayo wamesema kuwa wamefurahishwa kupata elimu hiyo ya anwani ya makazi na kwamba itawasadia kuinua biashara kutokana na kwamba itakuwa rahisi kutambulika eneo zilipo.
Post a Comment