Featured

    Featured Posts

BABA HALISI AAMURU FEDHA ZA SADAKA KWENYE SHUKRANI YA KUKABIDHI WATOTO KWA CHANZO HALISI ZIPELEKWE KUSAIDIA YATIMA

Na Bashir Nkoromo, Tegeta Namanga
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi ameagiza fedha zote za matunda (Sadaka) zilizotolewa na Uzao (Waumini) kwa ajili ya Shukurani ya kuwakabidhi Watoto kwa Chanzo Halisi (Mungu) kutoka kwa asili,  zipelekwe kusaidia Kituo cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

"Fedha hizi za matunda mliyotoa kwa ajili ya kuwakabidhi watoto hawa kwa Chanzo Halisi kutoka kwa asili, tutazipeleka kwenye kituo kimojawapo chenye hali ngumu sana cha kulea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu.

Mnajua vipo vituo vingi vyenye uhitaji wa kusaidiwa, lakini kuna kituo kimojawapo ambacho wana shida zaidi, paa la jengo lao linameharibika, sasa fedha hizi tutawapelekea ili waweze kuezeka wasinyeshewe na mvua, tukipeleka huko fedha hizi Chanzo Halisi atafurahi na kutubariki mno", akasema Baba Halisi.

Hayo yalijiri katika Ibada iliyofanyika Lango (siku) la 5 thebeti, 1 Majira Halisi (Jumapili Januari 8, 2023), Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga nje kidogo ya Katikati ya Jiji la Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na mamia ya Uzao ambao walifika na watoto kwa ajili ya Ibada hiyo.

Huku Baba Halisi akiwa amezungukwa na watoto tele baada ya kuwaita waje alipo, alisema "tumewaita watoto hawa kwa wingi namna hii kwa kuwa wale waliojulikana tangu asili sasa ndiyo wa chanzo halisi hivyo kila kitu kilichokuwa katika asili wakiwemo watoto hawa, kimerejea kwa kwa chanzo halisi, hivyo leo tunawakabidhi rasmi kwa Chanzo Halisi (Mungu).

Baada ya Adamu kukiuka, Watoto hawakupata kulelewa tena na Chanzo Halisi, ndiyo maana walifarikiana, wakawa watukutu, lakini sasa kwa kuwa kila kitu kimerejea kwa Chanzo Halisi watoto hawa atawalea mwenyewe na hawatagombana, kufarikiana wala kuwa na tabia mbaya tena", akasema Baba Halisi.

Mwanzoni mwa Ibada.
"Heriiii. Mliokombolewa Heri", Baba Halisi akasalimia Uzao, nao wakaitika "Heri Baba Halisi", Kisha akaendelea; "Nina furaha kukuona asubuhi ya leo. Leo Wazungu wanasema ni 'turning point', kwa maana ya, leo ni lango la kugeuka.  

Kila ambaye alikusudiwa bado alikuwa kwa namna moja au nyingine na yeye ni asili, maana ulizaliwa kwenye mazingira ya asili, ila kulingana na safari yoote tumekwenda na leo rasmi tumeachana naye asili. Mliona taa ikizima?, basi nilimuona kwa macho ikabidi akimbie!

"Kwa hiyo tulikuwa na Baba Halisi bado wa asili, Mama Halisi wa asili, Huduma Halisi wa asili, Udhihirisho Halisi wa asili, Utimilifu Halisi wa asili, Uaminifu Halisi wa asili, Moja halisi wa asili, Thamani Halisi wa asili, Fahari Halisi wa asili, Heri Halisi wa asili na woote hadi uzao Halisi walikuwa bado wa asili.

Ila leo tumekuwa wa Chanzo Halisi ili tufanye sherehe ya waliokombolewa isichukuliwe na wengine. Hata watekeleza Sauti bado walitekeleza ya asili ila sasa tunatekeleza ya Chanzo Halisi.

Baada ya kutoa ufafanuzi kwa undani kuhusu mada hiyo, Baba Halisi aliongoza shukurani kwa wote na vyote kufikia hapo na kuachana na asili, kisha baada ya Shukurani hiyo akafanya shukurani akaongoza shukrani ya kuinua toba.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi, Baba Halisi akifanya shukurani ya kuwainua Watoto kuwakabidhi kwa Chanzo Halisi (Mungu) kutoka kwa asili, wakati Ibada iliyofanyika Lango (siku) la 5 thebeti, 1 Majira Halisi (Jumapili Januari 8, 2023), Makao Makuu ya Kanisa hilo, Tegeta Namanga nje kidogo ya Katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Mada Kuu ya Ibada hiyo ilikuwa 'Kila kitu kimerudi kwa Chanzo Halisi'.
Mamia ya watoto kutoka maeneo mbalimbali wakipokea Shukurani (maombi) ya kuwakabidhi kwa Chanzo Halisi kutoka kwa asili, aliyokuwa akiwafanyia Baba Halisi wakati wa Ibada hiyo.                   Picha Zaidi👇
"Waleteni watoto wote waketi hapa mbele yangu, akasema Baba Halisi.
"Waketi hapo", akaelekeza.
Haida Halisi akimpanga vema mtoto mmoja wapo kati ya watoto walifika alipo Baba Halisi. Kulia ni Baba Halisi akieendelea kuhimiza watoto wote kusogea alipo.
Mwimbaji wa nyimbo za kumwinua Chanzo Halisi akiimba wimbo 'Hakuna kama Chanzo Halisi', wakati wa Ibada hiyo.
Mwimbaji mwingine akishiriki kuimba wimbo huo.
Mcharaza kinanda akinogesha wimbo huo.
"Sasa Watoto hapa ndiyo mahala penu, na leo ndiyo siku yenu, maana sasa kuanzia leo mtalelewa na Chanzo Halisi, hamtakuwa watukutu tena, wala kudokoa jikoni, wala kugombana,mtakuwa watoto wema, maana nanyi sasa mmetoka kwa asili na kuwa chini ya Chanzo Halisi mwenyewe", akasema Baba Halisi.
Baadhi ya Watoto waliofika kwenye Ibada hiyo wakimsikiliza Baba Halisi.
Baadhi ya watoto waliofika kwenye Ibada hiyo.
Baadhi ya Uzao wakiwa wamefika na watoto hata wachanga kwenye Ibada hiyo.
Uzao wakiwa kwenye Ibada hyo.
Mpuliza Domo la Bata nguli King Maluuu, akifanya vitu vyake wakati wimbo wa kumwinua Chanzo Halisi ukiimbwa.
Kingi Maluu na wenzake wakiendelea kutoa Burudani ya wimbo wa kumuinua Chanzo Halisi.
Watekeleza sauti wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Baba Halisi akiendelea kueleza umuhimu wa Somo alilokuwa akiendesha kwenye Ibada hiyo.
Baba Halisi akiendelea kufafanua jambo kwenye Ibada hiyo.
Uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo kwa unyenyekevu wa kutosha.
Uzao wakipepea vitambaa vyeupe kushangilia wimbo wa kumtukuza Chanzo Halisi uliokuwa ukiimbwa wakati wa Ibada hiyo.
Baba Halisi akipepea kitambaa kushangilia wimbo wa kumtukuza Chanzo Halisi uliokuwa ukiimbwa kwenye Ibada hiyo.
Moja Halisi na Kanisa wake (kushoto) wakiinua mikono kushangilia wimbo uliokuwa ukiimbwa kumtukuza Chanzo Halisi.
Baba Halisi akiendelea kuendesha Ibada hiyo.
Uzao akishangilia kwa furaha neno la Baba Halisi kwenye Ibada hiyo.
Baba Halisi akiwainua Watoto kwa kuwafanyia shukurani kwa kwenda kwa Chanzo Halisi kutoka kwa asili, wakati wa Ibada hiyo.
Kisha Baba Halisi akawarushia damu safi nyeupe (maji) kuwabariki watoto hao.
Baba Halisi akiendelea kuwabariki watoto hao kwa kuwarushia Damu safi nyeupe (Maji).
Kisha Baba Halisi akamzawadia mtoto ambaye amefikishwa kwenye Ibada hiyo.
Uzao wakiwa kwenye Ibada hiyo.
Kisha Ugeni kutoka Kibaigwa Dodoma, ukapata nafasi ya kusalimia. "Tumekuja kusalimia, na kuleta zawadi kidogo ya Lita 40 za mafuta kwa ajili ya kumtolea Chanzo Halisi", akasema kiongozi wa msafara huo.
Baba Halisi akiendesha Shukurani kwa Chanzo Halisi kusimamisha Uuumbaji na kisha akafunga Ibada hiyo.
Mama Halisi akiwa tayari kuondoka baada ya Ibada hiyo.
Baba Halisi (mbele) akiondoka Baada ya Ibada.
Baada ya Ibada: Watekeleza Sauti wanaoratibu Hija Halisi itakayofanyika Januari 29, mjini Kigoma, wakisubiri wanaojiandikisha kwenda kwenye hija hiyo.

Uzao wakiendelea kupumzika katika nyumba ya Ibada, baada ya Ibada kumalizika. 

Video: Baba Halisi akiwafanyia Shukurani watoto, wakati wa Ibada hiyo👇



 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana