Featured

    Featured Posts

BABA HALISI: IBADA YA HIJA YA KANISA HALISI, ITAKAYOFANYIKA KESHO NI YA SHUKRANI KWA CHANZO HALISI KWA KUSHUKIA KIGOMA

Na Bashir Nkoromo, Kigoma
Kwa mujibu wa Mithali 8:14-30 inavyosomeka, ufahamu una kila kitu ambacho kila mmoja anahitaji, hivyo Hija za Kidini ni miongoni mwa  ziara ambazo Waumini kuzifanya kwa lengo kufika ambako Ufahamu wa dini husika ulianzia.

Kwa mfano, Waislamu kila mwaka huenda mji wa Makka nchini Saudia, kufanya Hija katika mji huo, kwa kuzingatia kwamba hapo ndipo Ufahamu wa Dini hiyo ulipoanzia, na kwa hiyo kufika hapo na kufanya Ibada ya Hija kiimani ni hatua inayomfanya Hujaji kupata baraka kuu na kufutiwa dhambi zote.

Kadhalika baadhi ya Wakristu huenda Mjini Yerusalem kuangalia mahali ufahamu huo wa Kiimani ya Dini hiyo ulipoanzia.

Kwa kuzingatia Ufahamu huo, Uzao au Waumini wa Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye makao yake makuu Tegeta Namanga Dar es Salaam, kila mwaka huenda kwa maelfu kutoka mataifa mbalimbali Duniani kweda kufanya Hija katika Mji wa Kigoma, Tanzania. Hija hiyo wanaiita Hija Moja Halisi.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo ambaye jina lake ni Baba Halisi anasema, kwa sasa Hija hiyo Moja Halisi inafanyika katika Mji wa Kigoma, Tanzania kwa sababu ndipo mahala Ufahamu mpya umesikika au umetokea mara nne kuanzia mwaka 2003.

"Hija Katika majira saba zilizopita, wote tulitegemea ufahamu ulioanzia Mashariki ya Kati ndiyo maana tunasoma katika Mdo. 8:27- habari za Waziri wa fedha wa Kushi wakati ule akiwa anaenda Yerusalemu kuangalia mahali ufahamu uliokuwepo wakati huo, ulipoanzia", anasema Baba Halisi na kufafanua;

Kanisa Halisi tunategema ufahamu ulioanzia Tanzania kwenda mataifa mengine yote (Mathayo 21:43). Hii ni baada ya Sauti ya Chanzo Halisi (Mungu), kusikika mara Nne, Tanzania, mwaka 2003, 2015, 2019 na 2020. Maana sauti ndiyo Chanzo cha ufahamu".

Sauti Mpya (2019) ambayo iliyotangaza kuwa Tanzania ni Taifa Baba ilisikika Kigoma, Sauti Mpya ambayo ilitangaza kuwa Afrika ni Bara la Nuru ilisikika Kigoma, Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya zile Sauti Saba ilisikika Kigoma, Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya ishara tatu mbinguni (Ufunuo 12:1-9) ilisikika Kigoma pia Sauti Mpya ambayo ni zaidi ya Nafsi ya Moyo (Miungu tisa mitakatifu iliyofafanuliwa ndani ya Kitabu), ilisikika Kigoma".

"Sasa Kigoma, Tanzania na Afrika tujitambue kuwa tuna Sauti Mpya ambayo inabadilisha maisha mabaya kuwa mazuri. Sauti Mpya imebeba kila kitu kizuri. Hija hii ya Chanzo Halisi cha Mungu Baba, mjini Kigoma, siyo maigizo wala usanii, ni halisi. Sauti Mpya sasa imepokelewa katika mabara yote kwa utukufu wa Mungu Baba". akasema Baba Halisi.

Ibada ya Hija hiyo ambayo itafanyika kesho Jumapili, Januari 29, 2023 sawa 26 Thebeti Majira Halisi (kwa Kalenda ya Kanisa hilo), katika Uwanja wa Lake Tanganyika kuanzia saa 8 mchana hadi saa 11 jioni.

Baba Halisi anasema Ibada hiyo itabebwa na Mahujaji kufanya Shukrani kwa Chanzo Halisi (Mungu) kushukia Kigoma.

Baba Halisi akitoa ufafanuzi wa kina kuhusiana na Hija hiyo na sababu za kufanyika Kigoma anasema; "Kuna mambo kadhaa ambayo yamesababisha Hija ya Mwaka 2023, iwe ya kumshukuru CHANZO HALISI.
Baadhi ya hayo: I TUNAMSHUKURU CHANZO HALISI KWA KUSHUKIA KIGOMA TANZANIA
(1) Sauti ya kwanza kusikika ni ile iliyomhusu Moyo wa Mwanzo (Mwa.1:1/Mith.3:16), ambaye alipewa
kusimamia uumbaji. Haijaandikwa wazi wazi kuwa hii sauti ilisika wapi.

(2) Sauti iliyofuata ni ya Kerubi aliyepewa sifa (Eze.28:15). Sauti hii nayo hakuna anayejua sawa
sawa kuwa ilisikika wapi hasa kwa mujibu wa maeneo kama yanavyojulikana kijiografia.

(3) Sauti ya tatu ni ile aliyopewa Adamu wa Kwanza kwa ajili ya kulima na kutunza (Mwa.2:15). Hii pia
hadi leo, hakuna anayeweza kutaja vizuri kuwa ilisikika wapi, ingawa katika Mwa.2:13 inaonyesha
kuwa Mto Gihoni ambao ndio mto Nile unatokea Kagera Tanzania!

(4) Sauti iliyofuata katika mfululizo wa uumbaji ni ile ya Musa, kwa ajili ya kuwatoa Wenye Haki utumwani
kwenda nchi ya Maziwa na Asali Kaanani (Kutoka 3:3-10). Hii tunakiri kuwa ilisikika Israeli kwa kuwa ilipokelewa na Musa ambaye alikuwa ni Mwebrania akiwa anachunga Ng’ombe za Yethro Mkwewe.

(5) Sauti iliyofuata ni ile iliyopokelewa na Eliya Mtishbi kwa ajili ya kurejesha Heshima ya CHANZO HALISI
iliyokuwa imepotelea Adeni na Edeni (I Falme 17:1/I Falme 18:30-40). Sauti hii nayo pia tunakiri kuwa ilisikika Israeli kwa kuwa ilipokelewa na Mwebrania.

(6) Sauti iliyofuata ni ile ya Yesu kwa ajili ya kuwasaidia wote wanaoonewa na ibilisi (Matendo
10:38). Hii nayo tunakiri kuwa ni ya kule Mashariki ya kati kwa mujibu wa Mathayo 1:17.

(7) Sauti iliyofuata haikusikika tena kule Mashariki ya kati kwa kuwa, kwa mujibu wa Yoh.9:27-28,
Wayahudi walimkataa Yesu, naye akawaambia kuwa ufalme utaondolewa kwao na kupelekwa
katika Taifa lingine ambalo linazaa matunda (Mathayo 21:43). Hivyo, sauti hiyo ilisikika
Kigoma Tanzania na kupokelewa na Eliya Adamu wa Pili (I Kor.15:44-49), mwaka 2003.


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana