Featured

    Featured Posts

WANANCHI WAKUNWA NA KASI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI, TARURA WAMPONGEZA RAIS DK SAMIA

Mhandisi Aswile Mwasaga akimuelekeza jambo mmoja wa wahandisi wa TARURA wilayani Igunga kuhusuiana na ujenzi wa daraja lilopo kata ya Mwashiga
Na Odace Rwimo, Igunga

BAADHI ya wananchi wilayani Igunga mkoani Tabora wamefurahishwa na utekelezaji wa miradi inayotekelezwa na wakala wa barabara mjini na vijijini nchini (TARURA).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanachi wa kata ya Choma wilayani hapa wamesema tangu nchi hi ipate uhuru wamekuwa na shida ya barabara inayounganisha mkoa wa Tabora na shinyanga kupitia katana hapo kwan haikuwahi kupitika.
Juma Asawule na Hamisa Maganga ni wananchi wa kata ya Choma ambao walisimulia adha ya miaka zaidi 60 waliyoipata katika mto Manonga ambao unapita kijiji cha Mondo ukitenganisha kata ya Choma na Mkoa wa Shinyanga.
Walisema wamepoteza nguvu kazi nyingi kutokana na kupotelewa na wapendwa wao ambao wamepoteza maisha kupitia mto huo ambao sasa TARURA wameupatia dawa ya kudumu kwa kujenga daraja lenye midomo saba itakayosaidia sasa kuokoa maisha ya watu na kupandisha uchumi kazi.
Walisema wamekuwa wakipata tabu nyingi ikiwa ni pamoja na kuvuka mto huo ambao walilazimika kulipia sh.5000 kwa watembea kwa miguu huku pikipiki wakilipilia sh.10000 ili kuweza kuvuka kwa kutumia mtumbwi.
“Tunapenda kumpongeza rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyotujali sisi wananchi wake kwani amegusa maisha yetu moja kwa moja hasa kwa kututengenezea daraja hili na barabara inayoingia hapa kwetu kwenda Mkoani Shinyanga imepandisha uchumi wetu kwa kiwango kikubwa sana”Walisema wananch hao.
Meneja wa TARURA wilayani Igunga Mhandisi Aswile Mwasaga alisema serikali ya awamu sita imesaidia sehemu kubwa hasa katika kupandisha bajeti na kuwezesha TARURA kuweza kufanya kazi kwa kiwango kikubwa.
Daraja lilojengwa katika mto Manoga Kijiji cha Mondo kata ya Choma wilayani Igunga Mkoani Taboara kuunganisha Mkoa wa Tabora na Shinyinga
Kwa bajeti ya Mwaka 2022/2023 amabyo ilikuwa ni zaidi bilioni 1.9 ilisaidia sana kujenga madaraja na kufungua barabara ikiwemo barabara katika kata ya Nanga ambapo hapakuwepo miundombinu yoyote ya barabara katika kata hiyo.
Alisema kazi kubwa ilikuwa ni kujenga daraja la Mondo ambalo lilihgalimu zaidi milioni 500 ikiwa ni pamoja na ufunguzi wa barabara inayopita darajani hapo huku akibanisha bado ujenzi wa madarja mengine unaendelea sanjari na kufungua barabara ambazo hazikuwahi kutengenezwa ,akiongezea kuwa pia wamekamilisha ujenzi wa drasaja la Mwamashiga ambayo litaongeza uchumi wa kata hiyo.
Mhandisi Aswile alisema wanashukuru Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayofanya ya kuhakikisha miradi mingi inatekelezwa kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara hasa maeneo ya vijijini ambapo pamekosa huduma hiyo kwa kipindi kirefu.
Alisema kwa kipindi hiki wanafanya utekelezaji wa miradi mikubwa ambayo kipindi cha miaka ya nyuma miradi hiyo ilitekelezwa na wakala wa barabara nchini Tanroad pekee kutokana na ufinyi wa bajeti kwa wakala wa nbarabara za mijni na vijijini waliokuwa nao kwani walitegemea chanzo kimoja tu.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Igunga Sauda Mtondoo alimpongeza meneja wa TARURA wialyani Igunga kwa kazi nzuri anazofanya kwa uadilifu mkubwa wa kutekeleza mirdi kwa kufuata misingi ya kazi na thamani halisi ya fedha ikionekana katika miradi hiyo kwa sasa imeleta tija kubwa katika ustawi wa jamii.
Mtondooo licha ya kumpongeza Meneja huyo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kuwa kuendelea kuleta fedha za maendeleo katika wilaya ya Igunga,ambapo upande wa miundombinu ikiendelea kuimarika.
Alisema mji wa Igunga unakuwa wa kisasa kutokana na kupambwa kwa taa za barabarani na barabara za viwango vya rani kuzunguka mji huo ambao kwa miaka mingi ilikuwa ikizungukwa na barabara za vumbi hali ambayo iliondoa taswira ya mji huo.
Aliongeza kuwa kazi ya Rais ni dira kamili ya maendeleo ya Tanzania kuendelea kujikita katika ushindani wa kimataifa kwani miji mingi hapa nchini imekwa na mvuto wa kibiashara kutokana maendeleo ya miundobinu mizuri ya barabara.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana