Featured

    Featured Posts

MBUNGE DITOPILE AMPONGEZA RAIS SAMIA KUENZI MAONO YA BABA WA TAIFA HAYATI NYERERE






 MBUNGE wa Viti Maalum Mariam Ditopile Mariam amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kuruhusu mikutano ya hadhara kama namna ya kuenzi maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na dhana ya kukiimarisha chama.


Mariam amesema hayo Januari 26,2023, wilayani Kongwa katika kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM),ambayo yameandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Dodoma.


" mi nimefurahi mikutano hii kuruhusiwa ili wajulikane wenye pumba na mchele ni akina nani,jukumu letu ni kusimama na kusemea serikali na chama chetu,kwanza sasa hivi Rais amefanya mengi sana hata tukisimama kwenye majukwaa tuna mambo mengi ya kueleza,tuna mambo mengi ya kujivunia,"alisema.


Akizungumzia kuhusu maadhimisho hayo amewataka vijana kuzingatia …

[21:22, 1/27/2023] Sakina Uhuru Fm: MBUNGE wa Viti Maalum Mariam Ditopile amekishauri Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kujipanga vizuri kwa kutoa hoja zenye mashiko kwa kuwa kwa sasa Rais Samia Suluhu Hassan anajenga nchi.


Aidha,amewashauri madai ya Katiba mpya ya nchi yaanzie kwenye katiba ya Chama chao ambayo inaruhusu kiongozi mmoja kuwa mwenyekiti kwa miaka mingi bila ya kupokezana kijiti.


Mariam amesema hayo Januari 26,2023, wilayani Kongwa katika kuelekea maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi (CCM),ambayo yameandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Dodoma.


Alisema kwa sasa nchi inajengwa hivyo kama wana hoja watoe za kujenga nchi na sio za kuleta chuki kwa watanzania.


"CCM ina utaratibu wa kupokezana vijiti na wenyeviti wake wanajulikana,sasa leo niulize hii CHADEMA mbona kila siku mwenyekiti wake ni Freeman Mbowe?,kwani katiba yao ikoje,kwa nini sasa wasianze kuweka katiba yao vizuri ndio waje nje?,"alihoji mbunge huyo.


Aliongeza kuwa,"Juzi Makamu Mwenyekiti wao alirudi nchini,mi nikajua ana vitu vipya vya kuongea kumbe hakuna kitu anazungumzia katiba mpya,"alisema.


Aliongeza kuwa Rais Samia amejenga madarasa,vituo vya afya,amepeleka umeme na wananchi wanafurahia serikali yao.


" Wao wanatakiwa sasa hivi wakisimama watoe tiba mbadala lakini kama anataka kuleta hoja za Rais kutochaguliwa asubiri sana,sisi vijana,wanawake hatutakubali Rais wetu aguswe kiurahisi,"alisisitiza.


RUHUSA YA MIKUTANO YA HADHARA.


Mariam alimpongeza Rais Samia kwa kuruhusu mikutano ya hadhara kama namna ya kuenzi maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na dhana ya kukiimarisha chama.


" mi nimefurahi mikutano hii kuruhusiwa ili wajulikane wenye pumba na mchele ni akina nani,jukumu letu ni kusimama na kusemea serikali na chama chetu,kwanza sasa hivi Rais amefanya mengi sana hata tukisimama kwenye majukwaa tuna mambo mengi ya kueleza,tuna mambo mengi ya kujivunia,"alisema.


Awali,Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Abdulhabib Mwanyemba alikumbusha suala la kuanzisha miradi mipya na kuboresha iliyopo ili kuweza kujikwamua kiuchumi. 


Pia aliwaagiza wenyeviti wa wilaya kuhakikisha wanaanzisha mfumo wa kuwaandaa  chipukizi kupitia vituo watakavyoanzisha.


Shughuli mbalimbali zimefanyika katika sherehe hizo za kuelekea kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa CCM ikiwemo kupanda miti,kukagua ujenzi wa jengo la dharura katika hospitali ya wilaya ya Kongwa,kugawa kadi wa wanachama wa umoja huo na kupandisha bendera kwenye mashina 10.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana