Featured

    Featured Posts

DISMAS LYASSA APITISHWA KUWA MKUU WA MAWASILIANO MACHINGA MKOA PWANI, AMPONGEZA RAIS DK SAMIA KWA MILIONI 10

Mwandishi wa Habari Dismas Lyassa akiwa katika studio za TBC hivi karibuni ambako aliarikwa kutoa mada mbalimbali

MWANDISHI wa habari wa muda mrefu nchini ambaye amekuwa akifanya shughuli za ushauri wa masuala mbalimbali nchini, ndugu Dismas Lyassa amepitishwa rasmi na machinga kuwa Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano na Mafunzo katika Shirikisho la Machinga Mkoa wa Pwani (SHIUMA).
Katika kikao cha SHIUMA kilichokaa katika Ukumbi la Garden, wajumbe walipitisha kwa kauli moja kumwomba Dismas Lyassa awasaidie kukishika kitengo huku wakiamini kwamba kwa uwezo wake atawasaidia kuwasemea na hata kuwashauri katika masuala mbalimbali.
"Tumekuwa katika mazungumzo ya muda sasa na Dismas Lyassa, hatukuwa na uhakika kama angekubali kushika nafasi hii, lakini tulifurahi pale tulipomuhitaji kwa mazungumzo alikuwa anakuja," anasema Filemon Maliga, Mwenyekiti wa SHIUMA Mkoa wa Pwani.
Maliga anasema anao watu mbalimbali ambao aliwashirikisha kuhusu Dismas Lyassa, wengi walionyesha kumkubali Dismas wakimsifia kwa uimara wake katika masuala ya uongozi. Dismas nje ya kusomea na kufanya kazi za Uandishi wa Habari na vyombo mbalimbali vya ndani na nje ya nchi, pia amesomea Stashahada ya Uzamili katika Uongozi na Utawala aliyoitimu Aprili 2014 Chuo cha Utumishi wa Umma kilichoko chini ya Ofisi ya Rais (TAMISEMI).
Katibu wa SHIUMA Godfrey Lukas anasema imani yake ni kwamba SHIUMA sasa imepata msemaji ambaye atakuwa sio tu msemaji bali atasaidia kutoa mafunzo kwa machinga ili waweze kuwa na ufahamu kuhusu shughuli zao na kuziendesha ilivyo rasmi.
"Tulipozungumza na Dismas Lyassa na kisha kuwasilisha jina lake na sifa zake kwa machinga wengine katika shirikisho, wengi walionekana kumfahamu hasa kwa weredi wake katika kazi, ni imani yetu SHIUMA tutakwenda mbele zaidi," anasema Katibu Lukas.
Kwa upande wake Dismas Lyassa, anasema "Tanzania kuna watu wengi, kama ni wasomi na wenye sifa mbalimbali wapo wengi, kitengo cha kunipendekeza mimi kimenipa heshima na ninamshukuru Mungu, nitafanya kila ninachoweza kushirikiana ili kuimarisha machinga katika mkoa mzima wa Pwani, wilaya, kata na mitaa yake".
Lyassa anasema kuna shida kubwa ya taarifa sahihi..."Nitajitahidi kuwasaidia machinga wenzangu kuwafikia taarifa sahihi...kwa mfano SHIUMA tumepokea milioni 10 kutoka Serikali ya mama yetu, Rais wetu Dk Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mkoa Pwani...sio wengi wenye taarifa...wengine wanazungumzia kuhusu vitambulisho vya wajasiriamali, lakini vitambulisho vipo na vinaendelea kutolewa. Kikubwa naomba ushiriakiano pande zote ili tuweze kusonga mbele....umoja imara baina ya machinga, Serikali na Watanzania kwa ujumla ndio kufanikiwa kwetu".
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana