Featured

    Featured Posts

WATUMISHI WAJIMWAMBAFAI BAADA YA KUWAFUNGA WABUNGE 4-0 BUNGE BONANZA 2023+video

Nahodha wa timu wa Watumishi wa Bunge, Mussa Mlula akitamba baada ya kuwafunga wabunge mabao 4-0 katika mchezo wa soka huku baadhi wachezaji wa timu ya Bunge wakiongozwa na nahodha wao Chumi Cosato wakijitetea na kuahidi kufanya vizuri katika mabonanza yajayo.
Tambo hizo na utetezi huo umetokea wakati wa Bunge Bonanza 2023 lililofanyika Januari 28, 2023 kwenye viwanja vya Shule za John Merlini, Miyuji Jjijini Dodoma ambapo wabunge, watumishi wa Bunge na Baraza la Wawakilishi kutoka Zanzibar walishiriki katika michezo mbalimbali. Mdhamini Mkuu wa Bonanza hilo ni Benki ya NMB.

Majaliwa akimkabidhi Nahodha wa  timu ya soka ya Watumishi, Mussa Mlula  kombe la ushindi wa baada ya kuifunga timu ya Bunge mabao 4-0 wakati wa Bunge Bonanza 2023 kwenye viwanja vya Shule ya John Merlin, Miyuji jijini Dodoma Januari 28, 2023.
Majaliwa akikabidhi kombe la ubingwa wa jumla kwa Mwenyekiti wa Bunge Bonanza 2023, Mbunge Festo Sanga. Ubingwa wa jumla umekwenda kwa wabunge.
Mbunge wa Mchinga, Salma Kikwete (wa tatu kushoto) akiifurahia moja vikombe pamoja na baadhi ya wabunge.
Shindano la kula ubwawa
Shindano la kunywa soda
Mbunge wa Singida Mashariki akipokea kutoka kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kikombe cha ushindi wa kuvuta kamba.
Mbunge wa Nzega Vijijini, ambaye ni Nahodha wa mpira wa kikapu, Kigwangala akipokea kombe la ushindi wa mchezo huo.



 Wabunge wakifurahia kupata kombe la ushindi

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA

Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, Nahodha wa watumishi akitamba...

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana