Featured

    Featured Posts

WANANCHI MTAA WA MKOMBOZI KIBAHA MJINI WAOMBWA KUFURIKA UJENZI ZAHANATI FEB. MOSI

Anasi Bwanari, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkombozi

WANANCHI wa Mtaa wa Mkombozi, Kata Pangani katika Halmashauri ya Mji Kibaha, Pwani wameombwa kufurika kwa wingi siku ya tarehe mosi Februari mwaka huu kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Zahanati ya Mtaa huo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Mtendaji wa Mtaa huo Philipina Gandi, kila mwananchi katika mtaa huo anapaswa kutenga muda wake ili siku hiyo ya tarehe mosi Februari kufika kwa ajili ya kuanza kuchimba msingi wa ujenzi wa Zahanati.
Mtaa wa Mkombozi hauna Zahanati, hivyo ujenzi huo utawasaidia sana wananchi kupata huduma za afya ambazo kwa sasa wanalazimika kuzifuata katika mitaa mingine.
"Nina imani kubwa na wananchi wenzangu wa Mtaa wa Mkombozi, ni wananchi wenye ari kubwa sana ya maendeleo, tumetoka kumaliza ujenzi wa shule ya msingi ambayo pia hatukuwa nayo. Sasa nawakumbusha tena wananchi wenzangu kwamba tukutane tarehe moja mwezi wa pili ili tuchimbe msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Zahanati," anasema Anasi Bwanari, Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkombozi.
Kwa mujibu wa Bwanari, shughuli za uchimbaji msingi zinaanza rasmi saa moja asubuhi siku hiyo, azma ni kuhakikisha baada ya kuchimba watu waendelee na shughuli nyingine za kujiingizia kipato.
"Saa moja kamili tuwepo kwenye eneo letu la ujenzi wa Zahanati, tufanye kazi mara moja kisha tuendelee na mambo mengine yetu mengine," alisema Bwanari na kumuomba kila mwananchi wa Mtaa wa Mkombozi na mitaa jirani kuja kushirikiana kuhakikisha ujenzi huo unaanza kwa kasi.
Hivi karibuni wataalam kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha walitembelea eneo linalotakiwa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati na kulipitisha, ikiwamo kutoa ramani maalum ambayo ndiyo itafuatwa katika ujenzi wa Zahanati hiyo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana