NA MWANDISHI MAALUM, ARUSHA
Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt.Angelina Mabula ameiagiza bodi ya shirika la nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha shirika hilo linajenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya watanzania wa kipato cha chini.
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya kuzindua bodi mpya ya shirika hilo iliyofanyika jijini Arusha ambapo amesisitiza suala la kutumia teknolojia katika ujenzi wa nyumba hizo ambayo inatumia muda mfupi, gharama kidogo na nyumba imara.
Dkt. Mabula amesema ilani ya ya chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2020 - 2025 ni kujenga nymba 50,000 hivyo bodi hiyo ameipa jukumu la kuhakikisha malengo yanatimia.
"Ili jambo hili lifanikiwe la kujenga nyumba nyingi kutokana na mahitaji kuwa makubwa ni vyema mkatafuta watu mtakao ingia nao ubia ili kupata fedha zitakazo fanikisha ujenzi wa haraka" ameshauri.
Sambamba na hayo waziri Mabula amesema ni vyema ujenzi wa nyumba ukazingatia suala la maegesho ya magari kwani limekuwa ni tatizo kwa nyumba zilizopo mjini.
Dkt Mabula ameongeza kuwa tangu shirika hilo lianzishe miaka michache baada ya Tanzania kupata uhuru ni nyumba 20,000 tu zimejengwa wakati mahitaji ni zaidi ya 200000 hivi sasa. Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la nyumba NHC Nehemiah Mchechu amesema mpango walionao ni kubomoa nyumba zilizo chakaa maeneo ya katikati ya mji na kujenga maghorofa.
"Shirika linadai zaidi ya bilioni 20 lakini limejiwekea mikakati ya kukusanya madeni yake ambayo tunainani njia tutakayotumia tutafanikiwa" amefafanua Mchechu.
Amesema kuwa ili kuhakikisha shirika linaendelea kujua ndio maana mwishoni mwa mwakajana walizindua sera ya kushirikisha wabia hivyo maelekezo ya waziri kutafuta wawekezaji litafanyika ipasavyo.
Naye M/Kiti wa bodi hiyo Dkt. Sofia Kongela ameeleza kuwa mwelekeo wa shirika hivi sasa ni kuhakikisha linajenga nyumba za gharama watakazo mudu wananchi wa kipato cha kawaida na kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ule wa Samia housing scheme ambayo ni ya gharama nafuu.
Mbali na hilo pia amesema wako tayari kufanyia kazi maelekezo yote ya waziri waliyopewa ikiwemo wa kuhakikisha kuna maegesho kwenye nyumba zitakazojengwa.
Hata hivyo katika uzinduzi wa bodi hiyo wajumbe wamekabidhiwa nyenzo watakazo tumia kulifahamu vyema shirika hilo, dira iliyopo na namna watakavyotekeleza miradi mbalimbali.
Waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt.Angelina Mabula akimkabidhi vitendea kazi mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la nyumba la Taifa NHCMkurugenzi mtendaji wa shirika la nyumba la Taifa NHC Nehemiah Mchechu akionyesha waandishi wa habari baadhi ya miradi inayotekelezwa hivi sasa
Picha ya pamoja ya wajumbe wa bodi ya shirika la nyumba NHC pamoja na waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt.Angelina Mabula mara baada ya kuzindua bodi hiyo
Post a Comment