Featured

    Featured Posts

KATIBU MKUU CCM ATAKA DIRISHA MOJA LA MSAMAHA WA KODI MIRADI YA MAENDELEO

 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo.

-Asema vigingi kwenye msamaha wa kodi vinachelewesha

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amesema vigingi vilivyopo kwenye msamaha wa kodi vinachelewesha maendeleo, hivyo ametaka kuwepo kwa dirisha moja ambalo litakuwa linawajibika na miradi inayoingia nchini na kutakiwa kutekelezwa wa msamaha wa kodi. 

Chongolo ameyasema hayo Februari 1 mwaka 2023 alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kilombero akiwa kwenye ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi na kukagua uhai wa Chama mkoani Morogoro akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM). 

“Vigingi vya msamaha wa kodi vinakwenda kutuchelewesha , ni lazima tuwe na dirisha moja linalowajibika na miradi inayoingia nchini na kutaka kutekelezwa kwa msamaha wa kodi. Kama mradi una kigezo cha msamaha wa kodi basi kuwe na dirisha maalum linalohusika na kushughulikia miradi hiyo unapoenda kusainiwa na mkandarasi hilo tatizo lisiwe sehemu ya kikwazo. 

“Hatuwezi kuwa na Serikali moja msamaha wa kodi tunatoa wenyewe , mradi tunasainisha wenyewe halafu jambo moja la msamaha wa kodi linakuwa na kusaini mradi kunakuwa mbele. Nadhani tufike mwisho na hiyo isiwe hoja tena kwa wananchi kuanzia sasa hivi uwekwe mfumo wa kuhakikisha msamaha wa kodi hauwi kikwazo cha kufikia mwisho kwasababu mpaka inaitwa msamaha wa kodi maana yake ni ndani ya Serikali kumechakatwa mradi. 

“Tukakubaliana kwamba mradi utatekelezwa kwa kuondosha kodi na hasa ya ongezeko la thamani VAT maana yake sio kodi nyingine maana hizo zinakuwa zimelipwa kasoro VAT.Lazima twende tukashughulike na hilo kwa kulifuatilia na kuweka mambo vizuri,”amesema Chongolo.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana