Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba lenye makao yake Makuu Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, amesema yeye siyo Mtume wala Nabii bali ni Baba Halis, na kufafanua kuwa hao Chanzo Halisi (Mungu) alikuwa akiwatuma kwa kuwa majira ya kuja mwenyewe yalikuwa hayajatimia.
Amesema, mbali na kuwa siyo Mtume wala Nabii lakini pia hafanyi miujiza kwa sababu yeye ni Halisi, akifanya jambo linakuwa na kuhusu Mitume na Manabii akasema, kuwa hivyo ni hatari maana hao wote walipotokea hawakudumu.
Baba Halisi amesema hayo wakati wa Chakula cha mchana alichowaandalia Wafanyabiashara wa Tegeta Nyuki na kwa Ndevu, katika hema maalum aliloandaa katika Viwanja vya Nyuki, ambako tangu Jumapili iliyopita amekuwa akifanya mikutano ya ibada, ikiwa ni mara ya kwanza kwa Kanisa Halisi kufanya mikutano kwenye viwanja vya wazi tangu lilipoanza kuwepo takriban miaka mitano sasa.
Amesema, aliamua kuwaita kwa kuwa amependa sana wajue neema iliyopo katika eneo lao, maana wapo watu wengi wanaipata neema hiyo Tanzanaia na Duniani kote kutoka Kanisa Halisi kupitia mahubiri yake, ambayo huwafikia kwa njia mbalimbali za mawasilino, hivyo siyo vema wafanyabiashara hao kutoijua.
"Chakula hiki sikuwaitia kwa sababu yoyote, ila kwa kuwa ni majirani zangu, na nimetaka tukutane tuzungumze mlijue hili Kanisa Halisi lililopo katika eneo lenu lina neema gani, maana sasa hampaswi kwenda tena kwa waganga kutafuta utajiri, au kupata suluhu ya matatizo yakiwakumba.
Wewe ukiwa na tatizo au unahitaji biashara yako inyooke siende kwa mganga, njoo pale Kanisa Halisi, tupo wakati wote na tutakuhudumia bila kutoa pesa yoyote kwa sababu unastahili, maana sisi hatubagui, dini wala dhehebu lolote.", akasema Baba Halisi.
Baba Halisi alieleza msimamo wa mafundisho ya Kanisa Halisi kuwa ni Upende usio bagua, Utawala wa Amani na uzalishaji na baada ya kueleza sura ya Kanisa hilo alikaribisha maswali kwa yeyote aliyehitaji kujua chochote kuhusu Kanisa hilo.
Kufuatia kutoa nafasi hiyo watu kadhaa waliuliza maswali ikiwemo kutaka kujua kwa nini yeye anaitwa Baba Halisi, kwanini wanavaa jazi jeupe, je, yeye ni Mtume au Nabii na je amewahi kufanya miujiza yoyote? ambapo Baba Halisi alijibu maswali hayo kwa usahihi, na kuomba yeyote ambaye atataka kujua zaidi afike Kanisa Halisi na kupata ufafanuzi wa kina kutoka kwake au kwa watekeleza sauti.
Picha zaidi za tukio hilo kuanzia mwanzo👇
Baba Halisi akiwaangalia wakati wanakula na baada ya kula ndipo akaanza kuzungumza nao👇
m m mm
Post a Comment