Featured

    Featured Posts

BABA HALISI LEO IJUMAA, KUACHILIA KUBWA KULIKO MKUTANO WA IBADA YA WIKI YA UKOMBOZI WA MAISHA YAKO'.

Na CCM Blog, Tegeta Nyuki.
Baaba ya Baba Halisi kuachilia Baraka ya Mafuta ya Sauti kwa waliohudhuria Mkutano wa Ibada ya 'Wiki ya Ukombozi wa Maisha yako', uliofanyika katika jana katika Viwanja ya wazi vya Tegeta Nyuki, Dar es Salaam, leo anakuja na Sauti ya tajiri kuwa tajiri kuliko.

Katika Mkutano huo wa jana wa Ibada hiyo ambao ulikuwa wa tano tangu Kanisa Halisi la Mungu Baba lianze kufanya mikutano kwenye viwanja vya wazi tangu lilipoanza kuwepo miaka takriban mitano, Baba Halisi aliachilia Mafuta ya Sauti, na kila aliyekuwepo alionekana kupokea kwa shangwe kuu.

Baba Halisi alisema, Majira haya ni tofauti na yale yaliyopita ambayo mtu alikuwa akiomba hapati, majira ya sasa mtu akiomba kwa haki anapata ndiyo sababu aliamua kuachilia mafuta hayo ili kila aliyepokea apate baraka na kila atakachoomba.

"Sasa leo nitaachilia mafuta kupitia kinywa cha Baba Halisi (yeye), na mafuta haya ni zaidi ya chochote, ni zaidi ya hirizi na chochote cha kishirikina. Baada ya kupokea mafuta haya ya sauti hutapatwa tena na vibwengo, vinyamkera, hasira, aibu, maana yake hutaona tena kuachiwa na aliyekuumba.

Maana sasa Mungu atakaa moyoni mwako tofauti na kipindi kile cha waliotumwa ambacho Mungu hakukaa ndani ya moyo wako, mafuta ya sauti ukiyapokea nuru itatawala, utatembea katika barabara ya Chanzo Halisi ambayo haina Simba wala wanyama wakali", akasema Baba Halisi.

"Tena si hivyo tu, ukikishapokea Maji haya ya sauti utakuwa na moyo wa fedha, maana inatakiwa fedha tuzitawale siyo zitutawale, ukizishika zitulie uzitumie kwa fadida siyo kuzitapanya kuzipeleka kwa wachawi, uzinzi na ulevi, uharibifu wowote unaokukumba wote utafutika", akasema Baba Halisi.

Kuhusu kuachilia leo Sauti ya tajiri kuwa tajiri zaidi ambayo ataiachilia leo, Baba Halisi alisema, "Wewe mfanyabiashara, hata kama unaona ni tajiri lakini tambua kuwa ulipaswa kuwa tajiri zaidi ya hapo, sasa kesho nitaachlia sauti hiyo, na ninakuomba wewe mfanyabiashara wa Tegeta Nyuki na Tegeta kwa ndevu jihahidi ufike hapa, utaona".

"Lakini najua Wafanyabiashara wengi ni vigumu kufunga biashara zao na kuja hapa, lakini kutokana na kuwapenda kupitiliza nitatoa mwaliko kwa watu 100, kuwakaribsha Jumamosi  mje mahala hapa tushiriki (tule) chakula pamoja huku tukizungumza kwa nini mnatakiwa muwe matajiri kuliko, maana hii ni kwa mujibu wa Sauti ya Chanzo Halisi.", akasema Baba Halisi.

Mkutano wa leo (Ijumaa), utakuwa wa Sita, tangu Kanisa Halisi la Mungu Baba lilipoanza kufanya Mkutano wa kwanza Jumapili iliyopita.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, Baba Halisi akizungumza baada ya kuachilia Shukurani ya 'Mafuta ya Sauti', katika  Mkutano wa tano wa Ibada ya 'Wiki ya Ukombozi wa Maisha yako', uliofanyika jana Viwanja vya Tegeta Nyuki, Dar es Salaam.

Tazama hapo👇 Matukio zaidi yaliyojiri,

Faida Halisi akiendesha Ibada ya utangulizi na kufungua Mutano wa Ibada hiyo.
Baba Halisi mwenyewe akiendesha Ibada hiyo. Kulia ni Mnara Mmoja Halisi.
Kisha Waimbaji wa nyimbo za kumtukuza Chanzo Halisi wakaachilia wimbo ambao ulisisimua mkutano huo.
Minguu ya baadhi ya Uzao ikiwa hewani wakati wakicheza wimbo huo na kurukaruka kumtukuza Chanzo Halisi.
Kwa furaha Uzao akaamua kumbeba Uzao mpya, Denis mkazi wa Tegeta Salasala ambaye alianza kuhudhuria mkutano kama huo wa juzi. kwa mujibu wa yeye mwenyewe amekuwa akitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu lakini baada ya kuhudhuria mkutano wa Kanisa Halisi, ameacha.
Denis (kushoto) akisakata Wimbo na Uzao wa Kanisa Halisi. kwa mujibu wa yeye mwenyewe amekuwa akitumia dawa za kulevya kwa muda mrefu lakini baada ya kuhudhuria mkutano wa Kanisa Halisi, ameacha.
Faida Halisi akifurahi na Wanafunzi waliofika kwenye mkutano huo baada ya kutoka shule.
Mhudhuraiji wa Mkutano huo, akipiga mbija kufurahia wimbo.
Denis akiinua mikono kufurahia Baba Halisi
Kisha Denisi akapiga magoti kumshukuru Baba Halisi, baada ya Baba Halisi kumwambia "Ukiendelea kuwa hivyo bila kuwa teja, nitazidi kukupenda, hata Kanisa (mke) nitakupa.
Moja Halisi akimsaidia mwenye ulemavu ambaye alifika kwenye mkutano huo.
Mtekeleza Sauti (kulia) akifurahi Kijana ambaye alitaka kujua mambo kadhaa kuhusu Kanisa Halisi, naye Mtekeleza sauti huyo akamjibu kwa upendo mkubwa.
Baba Halisi akishuka jukwaani tayari kwa kuondoka baada ya kukamilisha ibada hiyo.
Akapanda gari lake na kuondoka. 

Ends

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana