Featured

    Featured Posts

BALOZI KALLAGHE AWAFUNDA MAAFISA HABARI, MAWASILIANO NA UHUSIANO WA SERIKALI, KUHUSU PROTOKALI

Na K-VIS Blog/Khalfan Said, Dar es Salaam
Mwanadiplomasia mahiri Balozi (Mstaafu) Peter Kallaghe, amejuza Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali (TAGCO) kwamba Itifaki au Protokali ni sehemu ya Uhusiano.

Balozi Kallaghe, ameyasema hayo leo akiwasilisha mada ya Protokali kwa Wajumbe wanaoshiriki Kikao Kazi cha 18 cha TAGCO, kilichoanza jana, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.

Katika Kikao kazi hicho cha siku tano, kinachowakutanisha Maafisa hao wapatao 600 kutoka Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, Balozi Kallaghe alisema, "Kazi ya tasnia yenu ni kufungua milango ambayo imefungwa, tabia ni moja ya njia bora ya kufungua milango iliyofungwa".

Balozi Kallaghe, aliwaeleza maafisa hao misingi mbalimbali ya kuzingatia katika Protokali ili kuonyesha ustaarabu katika ofisi wanazozitumikia, kuwa ni pamoja na dhima ya kuwashauri viongozi wao katika ushiriki wa matukio mbalimbali ndani ya ofisi na nje ya ofisi.

Alisema pamoja na wajibu mwingine Maafisa hao wanawajibu wa kuwashauri viongozi wao kuhusu  kuheshimu mialiko, muda, kwa kuwa hiyo ni ishara ya kuonyesha heshima ya shughuli husika .

“Lazima uonyeshe ustaarabu (etiquette), kwa kujua mambo ambayo kwa utamaduni wa sehemu fulani yanakubalika na yasiyokubalika.”Alibainisha Mwanadiplomasia huyo.

Balozi Kallaghe aliwaeleza pia umuhimu wa uchaguzi wa mavazi wanayovaa wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi na kuepuka mavazi yanayopiga kelele (shouting colors), akasema, “Unavyovaa ni sehemu ya weledi wako, kuelewa nguo gani unavaa na kwa wakati gani ni jambo la msingi".

Akieleza zaidi Balozi Kallaghe, ambaye ni mbobezi katika fani ya Mawasiliano alisema wanapaswa kujua utaratibu wa ukaaji (Seating arrangement) kwa viongozi wao, namna ya kuzungumza, lakini pia kutamka majina kwa usahihi.

Balozi (Mstaafu), Mhe. Peter Kalaghe akzungumza kwenye Kikao hicho.
Mkurugenzi wa Mawasiliano, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mindi Kasiga akizungumza kwenye Kikao hicho.
Balozi Kallaghe akiteta jambo na Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sara Kibonde.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Bw. Selestine Kakele ambaye ni Mwenyekiti wa Kikao, akiongoza majadiliano.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Msigwa akijibu baadhi ya hoja za washiriki.
 Bw. Kakele na Bw. Msigwa wakiteta jambo.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), David Misiime akifuatilia kwa makini mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye Kikao hicho 👇







'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
Mwenyekiti wa TAGCO, Bi. Sara Kibonde. akiteta jambo na mshiriki mwenzake wa kikao hicho.
Balozi Kallaghe akiwa katika picha ya kumbukumbu na Washiriki wa Kikao hicho. Kushoto ni Gerison Msigwa, Bw. Selestine Kakele, Balozi Mindi Kasiga na Bi. Sara Kibonde.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana