Na Bashir Nkoromo, Tegeta
Kanisa Halisi la Mungu Baba, leo limefanya Mkutano wake wa Ibada wa mwisho katika Viwanja ya Tegeta Nyuki, Dar es Salaam, Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo Baba Halisi akiwashukuru wakazi wa Tegeta yote, kwa ukarimu walioonyesha kwa muda wa siku nane ambazo Kanisa hilo limefanya mikutano yake kwenye Uwanja huo.
"Kwanza nianze kwa kuwashukuru wanachi wa Vitongoji vyote vya eneo hili la baraka la Tegeta, kwa namna walivyotufanyia ukarimu kwa siku zote nane tulizofanya mikutano yetu hapa.
Vyombo vyetu vya muziki vilikuwa vinalala hapa Uwanjani lakini sikusikia hata kuibiwa chochote, pia jana niliwakaribisha chakula cha mchana wakakubali kuja kwa wingi, nikala nao, basi Mungu awape baraka kupitiliza, eneo lote lizidi kuwa na amani, mabaya yote yafutike", akasema baba Halisi.
"Unajua Mungu anahimiza tuwe na Moyo wa shukurani, ndiyo maana lazima tuwashukuru hawa wakazi wa Tegeta, na leo somo nilikuja nalo ni 'Moyo wa shukurani', nataka kila mmoja apokee, asamehe bure hata aliyemkosea.
Hata kama aliyekuoa au uliyemuoa ni mkorofi leo mwambie nashukuru kuwa mwenza wangu, hata kama Bosi wako kazini ni mkorofi anakuandikia barua za onyo kila siku mtumie meseji umwambia unashukuru kufanya kazi kwake, ukishafanya hivyo utaona kuanzia leo anakupenda", akasema baba Halisi.
Baba Halisi akaenda mbali zaidi, akawaita mbele Watekeleza Sauti wa Kanisa hilo katika Nchi za Uganda, Kenya, Msumbiji na kuwataka leo waandike barua kwenda kwa Marais wa nchi zao, kuwambia 'nashukuru wewe kuwa Rais wangu'.
"Mimi pia leo nitaandika barua na nitampelekea Rais wangu kumwambia nashukuru yeye kuwa Rais wangu", akasema Baba Halisi, baada ya maneno hayo akashuka kunyunyiza damu safi nyeupe (Maji ya Baraka) kuzunguka eneo lote la makutano na abaada ya kurejea jukwaani akawaaga makutano na kuondoka.
Baba Halisi akizungumza katika mahubiri yake kwenye Ibada ya Mkutano wa nane na wa mwisho uliofanyika Viwanja vya wazi vya Tegeta Nyuki, Dar es Salaam, leo jioni.
Waimbaji wakiimba wimbo wa kusisimua wa kumsifu Chanzo Halisi, kabla ya Baba Halisi kutoa somo la 'Moyo wa skurani.
Wapiga ala wakizicharaza ala zao kunogesha wimbo huo. Uzao wakaanza kuserebuka kwa furahia wimbo huo👇
==================================================
Baba Halisi akaanza kufanya shukurani ya kuachilia 'Moyo wa Shukurani' huku jasho likimtoka.
Uzao na Watekeleza sauti wakipokea Shukrani hiyo.ya 'Moyo wa Skukurani'.
Mama Halisi akipokea kwa hisia nzito shukurani hiyo ya 'Moyo wa Shukurani'
Uzao wakipokea Skurani hiyo ya 'Moyo wa shukrani'
Baada ya kumaliza kufanya Shukurani kwa Chanzo Halisi, Baba Halisi akaita Uzao wote mbele yake wakiwemo Watekeleza sauti wa Nchi za Kenya, Msumbiji, Uganda na Kenya, kila aliyepo kwenye Ibada hiyo atoe shukurani kwa kila anayemfahamu hana kama ni mkorofi, au anamfanyia ubaya wowote. "Kila mmoja wenu amtumie ujumbe kumshukuru yeyote anayemhusu au kumjua hata kama mtu huyo ni mkorofi kwake. Ninyi watekeleza Sauti kila mmoja amwandikie barua Rais wa nchi yake kesho ampelekee, Hata mimi leo namwandikia Mheshimiwa Rais wangu kumshukuru", akasema Baba Halisi.
Watekeleza sauti wa nchi za nje zikiwemo Kenya, Msumbiji, na Uganda wakipokea maelekezo ya Baba Halisi.
Mama Halisi akipokea Shukurani ya Moyo wa skurani.
Kisha Baba Halisi akashuka jukwaani na kuanza kunyunyiza damu safi nyeupe (Maji) ya Baraka kuzunguka eneo lote la makutano.
Kisha akarejea tena Jukwaani kuaga kabla ya kuondoka.
Baba Halisi akaaga makutano kisha akachukua kila kilicho chake.
Akashuka kutoka jukwaani.
Akapanda gari lake na kuondoka.
Post a Comment