Featured

    Featured Posts

KILELE CHA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE KUFANYIKA APRILI 13, 2023

 









"Katika kila nyanja mshindi wa kwanza atapewa kitita cha Shilingi milioni 10, wa pili milioni 7 na wa tatu milioni 5. Wengine 7 wataungana na hawa watatu jumla 10, kila mmoja atapewa cheti cha kutambuliwa," amefafanua Waziri Mkenda.


Mhe. Ali Abdulgulam Hussein, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar akizungumza katika kikao hicho amesema  mkutano na wanahabari umefanyika Zanzibar kwa kuwa tuzo hizo zinahusisha pande zote mbili za muungano.


"Mkutano huu kufanyika huku Zanzibar ni kuonesha kuwa hizi wizara zetu mbili zinafanya kazi kwa ushirikiano na hili suala linahusu waandishi bunifu kutoka pande zote mbili," amesema Mhe. Ali Hussein.


Kwa upande wake Prof. Carolyne Nombo, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia amesema Wizara ina lengo kubwa la kuimarisha uandishi na uchapishaji hivyo ubunifu wa Tuzo utakuwa endelevu na mwaka huu Wizara imetenga zaidi ya Shilingi bilioni moja kwa ajili ya utekelezaji wake.


"Kwa kutambua thamani ya tuzo hizi, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya tuzo hizi kwa kuwa zitakuwa endelevu," amesema Katibu Mkuu Nombo.


Naye Prof. Penina Mlama Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo amesema tuzo hiyo imepokelewa kwa mwamko mkubwa sana kwani zilizinduliwa Septemba 2022 ,  miswada ikapokelewa hadi Novemba 2022 na ndani ya muda huo mfupi jumla ya mawasilisho 283 yamepokelewa.


"Tumefurahishwa sana na mawasilisho tuliyopokea sababu waandishi  kutoka maeneo na kada mbalimbali Bara na Visiwani wameshiriki, wakiwemo wakulima, Wafanyakazi, wafanyabiashara, wanazuoni na waandishi wachanga," amesema Prof. Mlama.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana