Na Mwandishi Maalum, Chato
Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais Tanzania Hayati Dk. John Magufuli amesema mambo ya kisasa hasa ya mitandao yamekuwa yakitengua mawazo chanya ya wasichana, na kuwashawishi waishi maisha ya mtandao ambayo mengi siyo maisha halisi.
Amesema pamoja na kuwepo umuhimu wa matumizi ya mitandao kwa ajili ya mambo yenye umuhimu, ni lazima inapowabidi kuitumia wafanye hivyo kwa umakini mkubwa ili kuepuka wakati wote yale ya hovyo na yanayowapotosha.
Mama Magufuli ameyasema hayo leo, katika hafla ya kuwakabidhi taulo za kike na baiskeli za magurudumu matatu kwa wasichana wa shule tattu za Sekondari za wasichana zilizopo katika Wilaya ya Chato, hafla iliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita.
“Kwa hiyo binti zangu elekezeni akili, maarifa na juhudi katika masomo na sio mambo mengine yanayoweza kuathiri maendeleo yenu kimasomo kama vile mambo ya mitandao ambayo mengi sio yenye kuonesha maisha halisi”, akasisitiza Mama Magufuli.
Akiongeza msisitizo, Mama Magufuli amewaasa Wanafunzi wasichana katika Shule zote za Msingi na Sekondari nchini kuhakikisha wanajiepusha kabisa na mambo yanayoweza kuathiri maendeleo yao kimasomo.
Mama Janeth Magufuli, mjane wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Tanzania Hayati Dk. John Magufuli, akikabidhi kwa furaha kasha lenye tatulo za kike kwa wanafunzi, nyumbani kwake Chato mkoani Geita, leo Machi 18, 2023.
Post a Comment