Featured

    Featured Posts

RC SENYAMULE AFURAHIA UWEKEZAJI WA KIWANDA KIKUBWA CHA SIMENTI DODOMA+video

 


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule ameshuhudia utiaji saini mkataba wa makubaliano ya ujenzi wa kiwanda kikubwa cha uzalishaji simenti wilayani Kongwa , Dodoma.

Makubaliano hayo wa ujenzi wa kiwanda hicho kitakachokuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani milioni moja kwa mwaka na kuanza kuajiri wafanyakazi 5000 yamesainiwa na viongozi wa kampuni zilizoingia ubia ambapo kwa upande wa Tanzania alisaini Mkurugenzi wa Kampuni ya Alotab & Block BB, Abdul Hillary Ally (kushoto) na Mwenyekiti wa Kampuni ya Libyan Petrolium ya Libya, Dmjed Rajab (kulia).
Hafla imefanyika Machi 17, 2023 mbele ya wajumbe wa Baraza la Ushauri Mkoa wa Dodoma (RCC) jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Kampuni ya Alotab & Block BB, Abdul Hillary Ally (kushoto) akitia saini mkataba huo.



Wakibadilishana hati
Mkurugenzi wa Kampuni ya Alotab & Block BB, Abdul Hillary Ally akitoa neno la shukrani kwa serikali.

Mwenyekiti wa Kampuni ya Libyan Petrolium ya Libya, Dmjed Rajab akitoa neno la shukrani kwa serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule  akielezea furaha yake kwa kampuni hizo kuamua kuwekeza kiwanda hicho Dodoma na kwamba kitasaidia kuleta ajira na kuinua pato la mkoa huo na Taifa kwa ujumla.

PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA


Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza kupitia clip hii ya video, wabia hao wakielezea sababu zilizowafanya wawekeze Dodoma...

IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA 
MHARIRI BLOG YA TAIFA YA CCM 
0754264203
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana