Featured

    Featured Posts

RAIS DK, MWINYI AONYA VIONGOZI WATAKAOWATISHA WATOA TAARIFA KUPITIA MFUMO WA SEMA NA RAIS MWINYI (SNR)

Ikulu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka viongozi  wa umma   kuwajibika kwa kero na changamoto wanazowasilishiwa na Wananchi kupitia mfumo wa Sema na Rais (SNR).

Amesema  wapo baadhi ya viongozi  wasiotaka kutatua  changamoto hizo kwa vile hawaoni umuhimu wake na akawaonya kuwa atawachukulia hatua. 

Rais Dk. Mwinyi halikadhalika amebainisha kupitia mfumo huo kuna utambuzi wa kitakwimu kujua kiongozi au taasisi zisizofanya vizuri na sasa wakati umefika kila mmoja aone umuhimu wa kuwajibika.

Ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport  kwenye kikao kazi  cha maadhimisho ya miaka miwili tangu kitengo cha Sema na Rais Mwinyi (SNR) kilichopo chini ya Afisi ya Rais Ikulu, kilipoanzishwa.

Rais Dk. Mwinyi akizungumzia mafanikio ya mfumo wa SNR kwa kipindi hicho cha miaka miwili alisema mfumo huo umeleta tija kwa wananchi ambao changamoto zao zimetatuliwa kwa kiasi kikubwa na mfumo ataendelea kuusimamia vema.

Alizungumzia pia suala la taarifa za ubadhirifu wa mali za umma na akaonya asitokee Kiongozi yeyote kuwatisha wanaowasilisha kero au changamoto kupitia mfumo wa SNR na akaahidi hatua zitachukuliwa dhidi ya kiongozi huyo. Ameahidi mtoa taarifa atalindwa na kuwaambia maafisa wa SNR wafanye kazi zao bila woga.

Vilevile, Rais Dk. Mwinyi alieleza kuthamini uhuru wa Mahakama na Serikali itayafikisha mbele ya haki matatizo yatakayopelekwa na  SNR  Mahakamani kwa Jaji Mkuu ayashughulikie na kuondoa kasoro zinazojitokeza.

Katika msingi wa utawala bora Rais alibainisha Serikali haina haki kuingilia mhimili wa Mahakama ila ina wajibu kuwasilisha changamoto wazishughulikie. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akihutubia katika Kikao Kazi cha  Maadhimisho ya miaka miwili ya Mfumo wa Sema na Rais (SNR), kilichowashirikisha maofisa wa Taasisi mbali mbali za Kiserikali, kilichofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip, mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar, leo. (Picha na Ikulu, Zanzibar).
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana