Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akihutubia wakati wa uzinduzi wa Programu ya Benki ya NMB ya mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya kati na juu katika hafla iliyofanyika Machi 14, 2023 jijini Dodoma.
Profesa Mkenda ameipongeza benki hiyo kwa kuanzisha mikopo hiyo itakayoisaidia serikali kwa asilimia kubwa katika uboreshaji wa elimu nchini pamoja na kuongeza wigo wa wanafunzi wengi kujiunga na vyuo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna akielezea jinsi watakavvokuwa wanatoa mikopo hiyo ambayo kwa mwaka wametenga sh. bil. 200 itakayotolewa kwa wazazi wafanyakazi wenye akaunti za NMB ambapo benki itakuwa inalipa moja kwa moja kwenye akaunti za shule wanakosoma watoto wao. Ametaja riba ya mikopo hiyo kuwa ni asilimia 9.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo akisema neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha Waziri, Prof. Mkenda.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Prof.. Kitila Mkumbo akielezea umuhimu ya mikopo hiyo iliyoanzishwa na benki hiyo na kwamba itasaidia kwa kiasi kikubwa kuziba pengo lililokuwepo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Nsolo Mlozi akitoa neno la utangulizi wakati wa hafla hiyo.
Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wakishiriki hafla hiyo.
PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Post a Comment