Katibu Mkuu Wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Liu Jianchao leo jijini Beijing nchini China.
Viongozi hao walibadilishana mawazo kuhusu utekelezaji wa makubaliano muhimu yaliyofikiwa na viongozi wakuu wa vyama na nchi hizo Novemba mwaka jana wakati wa Ziara ya Kiserikali ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan nchini China.
Pia walikubaliana kuimarisha mawasiliano na ushirikiano baina ya vyama, na kukuza maendeleo ya uhusiano kati ya China na Tanzania.
Katibu Mkuu Wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo amewasili jijini Beijing nchini China kwa ziara ya kikazi akiwa ameambatana na baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ya CCM.
Zifuatazo ni piha za matukio mbalimbali Katibu Mkuu Chongolo alipokutana na Waziri huyo wa China👇
Post a Comment