Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, jana aliendelea kudhihirisha kuwa Uongozi ni vitendo baada ya kutekeleza ahadi yake ya kuipatia gari Kampuni ya Magazeti ya Chama Uhuru Publications Limited (UPL), wachapishaji wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, kwa lengo la kurahisisha ufanisi katika utendaji kazi.
Chongolo alitoa ahadi ya kutoa gari hilo mapema Aprili 15, 2023 alipokuzungumza na wafanyakazi wa vyombo vya Habari vya Chama, katika ziara yake ya kustukiza iliyomuwezesha kukutana na wafanyakazi hao, akiambatana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Sophia Mjema.
Akizungumza baada ya kukabidhi gari hiyo aina ya Toyota Landcluser, Mkuu wa Utawala Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Mariam Msengi, alisema amekabidhi kutekeleza ahadi ya Katibu Mkuu Chongolo kufuatia dhamira njema aliyonayo ya kuviwezesha vyombo vya habari vya chama.
Akipokea gari hiyo katika hafla iliyofanyika nje ya Ofisi hiyo Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mkurugenzi wa vyombo vya habari vya CCM, Shaaban Kisu, alimshukuru Chongolo kwa kutekeleza ahadi yake, huku akisema gari hilo litaongeza nguvu na ufanisi katika utendaji kazi.
Katika hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa pia na Naibu Mhariri Mtendaji ambaye pia ni Kaimu Mhariri Mtendaji Ramadhani Mkoma, Kisu alisema UPL itaendelea kuchapa kazi kwa juhudi, maarifa na weledi na kwamba haitamuangusha Katibu Mkuu Chongolo, na CCM kwa ujumla.
Post a Comment