Featured

    Featured Posts

M-NEC HAMOUD: RAIS SAMIA KUPELEKA RIPOTI ZA CAG NA TAKUKURU KAMATI KUU AMEIPA THAMANI CCM, KIBAHA VIJIJINI WATOA TAMKO KUMPONGEZA

Bashir Nkoromo, CCM Blog, Mlandizi
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Jumaa, amesema, hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan, kupeleka Kamati Kuu ya CCM ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali (CAG) na ya Taasisi ya kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) inastahili kupongezwa kwa kuwa imekipa thamani Chama.

Amesema, hatua hiyo inastahili kupongezwa kwa sababu Rais Samia ambaye pia ni Mweneyekiti wa CCM, baada ya kupokea ripoti hizo angeweza kunyamaza na kutoa maamuzi peke yake kama Rais, lakini kwa busara yake akarudi kwenye Kamati kuu nayo ikajadili taariza hizo kwa kina na kutoa tamko.

"Mimi nadhani na sisi tujifunze kama Mwenyekiti wetu wa CCM, baada ya kutokea tukio hili akarudi kwenye Chama na sisi huku tuna nafasi kama hiyo, yaani sisi Madiwani, Mwenyekiti wa wilaya, kama Kuna jambo halijakaa vizuri ni vizuri tukakaa kujadiliana na kuona nini chakufanya kwa pamoja ili kuweza kusaidia Chama chetu kiweze kwenda vizuri, hili ni jambo jema" akaisema Jumaa.

MNEC Hamoud amesema hayo katika Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha vijijini kilichofanyika leo, kumpongeza Rais Samia kwa kutoridhishwa na utendaji wa taasisi za Serikali kutotimiza wajibu wake ipasavyo katika baadhi ya maeneo kama ukusanyaji mapato usioridhisha na  baadhi ya Watumishi wa Serikali kutokuwa waaminifu na waadilifu, hali inayosababisha Wananchi kuona Serikali ya CCM imeshindwa kusimamia vyema suala la Uadilifu kazini.

Amewashukuru CCM Kibaha vijijini kwa kuwa wa kwanza kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Rais Samia kwani anastahili kupongezwa kwa kazi nzuri anazofanya.

"Kwa hizi pongezi, tunapompongeza Mheshimiwa Rais anaona kwamba hajakosea ni jambo jema lakini tunapokaa kimya tunakuwa hatujampa nguvu lakini sisi Kibaha vijijini tunamtia nguvu na tunamsapoti kwa asilimia mia moja kwa kazi nzuri ambazo amefanya katika nchi yetu katika kipindi cha miaka miwili" alisema Hamoud.

Katika Kikao hicho kilichofanyika Ofisi ya CCM Kibaha Vijijini, Mlandizi, Chini ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo Mkali Kanusu, kilimalizika kwa kutoa tamko la kumpongeza Rais Samia kwa kutoridhishwa na baadhi ya maeneo, utendaji wa taasisi za Serikali kutokutimiza wajibu wake ipasavyo kama vile ukusanyaji wa mapato usioridhisha na  baadhi ya Watumishi wa Serikali kutokuwa waaminifu na waadilifu hali inayosababbisha Wananchi kuona kwamba Serikali ya CCM imeshindwa kusimamia vyema suala la Uadilifu kazini.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kibaha Vijijini mkoa wa Pwani Mkali Kanusu,Vijijini akizungumza katika Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya hiyo, kilichofanyika leo katika Ofisi ya CCM  Mlanizi, leo kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan. Kushoto ni Mumbe wa NEC Hamud Jumaa na kulia ni Katibu wa CCM Kibaha Vijijini Bernard Ghaty.
Mjumbe wa NEC Hamoud Jumaa (katikati) akiwa na baadhi ya Viongozi na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini baada ya Kikao hicho cha kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan, leo.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana