Na Yahya Msangi
Nianze kwa kusema teknolojia ya nano (nanotechnology) inatumika kwa bidhaa mbalimbali mfano nguo, matairi, rangi za kuta na magari, bodi za ndège, Meli, treni na magari, sementi, miwani, vipodozi, n.k.
Nano ni Nini?
Ili kujua nano ni nini chomoa kope yako Moja ikatekate vitoke vipande milioni Moja. Kipande kimoja ndio kina ukubwa wa nano. Kwa hiyo teknolojia ya nano ni kutengeneza bidhaa yenye udogo usioweza kuonekana kwa macho au hata darubini za kizamani. Katika fizikia kitu kikiwa kidogo kinakuwa "more active". Ndio maaana Bomu la nuklia lina madhara makubwa. Ni kwa kuwa Bomu la nuklia ni mkorogo wa chembechembe Ndogo kiwango cha nano. Hâta watu wafupi ni machachari kuliko watu warefu. Wana chembe ndogo kuliko warefu. Usigombane na mtu mfupi utakoma. Mtizame Lissu. Short and stout! Kipapa! Hawatuliagi.
Ukivaa nguo iliyotengenezwa kwa teknojia ya ngano unaweza kutembea kwenye mvua na usilowe. Baadhi ya majeshi yanawapa askari vitani. Kuna taulo za wamama nazo akiivaa hailowi.
Kuna rangi ukipaka nyumba haichakazwi na mvuta wala jua. Nyingine Huwezi kuandika juu yake. Ulaya Kuna tatizo kubwa la matusi kuandikwa ukutani. Rangi zenye nano ndio dawa. Hâta wale wa kutumia kinyesi kuandika matusi ukutani chooni nao wamebanwa.
Kuna matairi yana nano. Nayo ni imara sana. Licha ya nano kuwa na Faida pia Kuna madhara haswaa kwa afya. Sehemu kubwa inatokana na vipodozi vyenye nano.
Kwa kuwa nano si chembe asili Bali za kutengeneza basi ni rahisi mno kupenya kupitia pua (inhalation), ngozi (absorption), mdomoni (ingestion), macho (occulation absorption) na tumbo la uzazi (utérus absorption). Nano ni Ndogo mara milioni kuliko chembechembe za mwili (cells). Mfano mama mjamzito akiingiliwa na nano mwilini nano zitapenya ukuta wa tumbo la uzazi na kuingia kwa kichanga.
Nano inaweza kufanya Mtoto au hâta mtu mzima awe nyumbu (mjinga). Ukimwambia asile hadi afe habishi! Ukimwambia unafufua hâta kama wéwé unazika wafu wako anaamini. Anaacha kulima anapiga deki lami!
Miaka 5 iliyopita nilipata ka asali. Kutafiti uwepo wa bidhaa zenye nano (vipodozi, nguo , vifaa vya ujenzi na matairi) nchi za ECOWAS. Nilikuta ziko kibao. Hapa nimeweka picha ya vipodozi vyenye nano. Unapaka jumatatu jumanne unakuwa mzungu pori! Najua hâta Tanzania vipo na mnatumia kenge nyie!🤪🤪🤪.
Wee subiri utakuja kujuta baadae! Usije kudai sijakwambia?
Post a Comment