Featured

    Featured Posts

MKUTANO MKUU KANISA HALISI KUFANYIKA MWEZI UJAO, BABA HALISI KUTAJA MKURUGENZI ONE UP COMPANY ITAKAYOZINDULIWA RASMI SIKU HIYO

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Tegeta
Mkutano Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba, utafanyika mwezi ujao, ambao pamoja na mambo kadhaa, Kampuni ya Kanisa hilo ya One Up itazinduliwa rasmi na pia Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo ndani na Nje ya Tanzania Baba Halisi atataja Msimamizi Halisi wa kampuni hiyo.

Akizungumza katika Ibada iliyofanyika Juzi, Jumapili, Kao Kuu la Kanisa hilo, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, Baba Halisi aliyeendendesha Ibada hiyo, alisema Mkutano huo wa kila mwaka, mwaka huu utafanyika Mei 7, 2023 sawa na 12 Abibu Majira Halisi kwa Kalenda ya Kanisa Halisi.

Baba Halisi alisema, tofauti na mikutano iliyofanyika majira zilizopita, Mkutano huo utahudhuriwa na wajumbe watano kutoka kila mkoa hapa nchini na nchi za nje wakiongozwa na Mtekeleza Sauti wa mkoa au nchi husika.

Kufuatia utaratibu huo, Baba Halisi aliwaagiza Watekeleza Sauti (Wakuu wa Vituo vya Kanisa Halisi) wote katika mikoa pamoja na wao kufika kwenye mkutano huo na Uzao (Waumini) wanne na kuelekeza kuwa waumini hao wachaguliwe na waumini wenzao, wasiteuliwe na Watekeleza Sauti.

"Mkutano huu, kama ilivyo kawaida yetu utakuwa hauna siri na ndiyo maana huwa tunawakaribisha watu wote hata wasiokuwa waumini wa Kanisa hili maana ni Kanisa la Kijamii, kwa hiyo nawaagiza watekeleza Sauti mje hapa na wawakilishi wanne wa Uzao kutoka kwenye vituo vyenu, wawakilishi hao wachaguliwe na wenzao, msiwachague ninyi", Baba Halisi akasema na kusisitiza.

Baba Halisi akasema, Wajumbe mahsusi wa Mkutano huo watakuwa ni wale wa Vituo vya Kanisa Halisi ndani ya Tanzania, lakini wale wa Vituo vya nje watahudhuria mkutano huo kama wasikilizaji, kwa kuwa nao watakuwa na mikutano yao mikuu kila nchi.

"Watekeleza sauti wa Vituo vyetu vya Nchi za nje watakuja hapa kama 'Obsevers', maana wao watafanya mikutano yao mikuu huko, isipokuwa kila watakapofanya Moja Halisi atakufika. Wakifanya Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Msumbiji, Zambia, Marekani na kwingineko kote Moja Halisi itabidi lazima awepo na hatachoka kuwepo.", akasema Baba Halisi.

Baba Halisi alisema, kama ilivyo desturi kwenye Mkutano huo Mkuu Mada mbalimbali zitajadiliwa hasa kuhusu mwenendo na maendeleo ya Kanisa Halisi, ikiwemo kujadili rasilimali mapato na matumizi, kwa uwazi halisi.

Baba Halisi akasema, moja ya jipya litakalojitokeza ni uzinduzi rasmi wa Kampuni ya One Up, ambayo imeanzishwa na Kanisa Halisi hivi karibuni, ikianza kwa kutengeneza maji ya kunywa ya One Up, ambayo baada ya uzinduzi huo mbali na maji itazalisha bidhaa nyingine tano.

Alizitaja bidhaa hizo kuwa ni Sabuni ya maji ya One Up ambayo itakuwa inafaa kwa matumizi mbalimbali, Mafuta ya mgando ya One Up ya kujipaka yenye Alovera, Sabuni maalum ya One Up ya kunawia au kutakasa mikono, sabuni maalum ya Une Upa ya kusafisha sakafu za 'tiles' na Dawa ya One Up na kuondoa madoa.

Katika Ibada hiyo Baba Halisi mbali na kutangaza mkutano huo, pia aliendelea kusisitiza suala la Uzalishaji mali, ambapo alisema, Mwalimu aliyekuwa akiwafundisha Uzao mambo ya ujasiriamali kwa zaidi ya siku kumi hapa makao makuu ya kanisa hilo, sasa atakwenda kufundisha vituo vya mikoani na kuwataka uzao na watekeleza sauti kumpokea kwa upendo mkubwa.

Baada ya hayo Baba Halisi alikamilisha ibada kwa kutekeleza azma halisi ya ibada ya siku hiyo ambayo ilikuwa KUPOKEA MBEGU YA SAUTI NA KUPAKWA MAFUTA YA UZIMA WA UMILELE.

Katika Mada hiyo ya Ibada, pia Baba Halisi alifafanua kwa kina kwa nini Kanisa Halisi linafundisha Uzao (Waumini wake) kuabudu CHANZO HHALISI badala ya kuabudu MUNGU.

Alisema, inatakiwa kumwabudu Chanzo Halisi kwa kuwa ndiye anayestahili kuabudiwa kwa kuwa ndiye Muumba halisi wa yote na vyote katika nchi lakini Mungu siye jina halisi la alyeumba yote na vyote kwa kuwa wapo wengi walioitwa Mungu lakini hawakuwa wameumba chochote.

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Halisi la Mungu Baba na vituo vyote vya Kanisa hilo ndani na nje ya Tanzania Baba Halisi akiendesha Ibada iliyofanyika Kao Kuu la Kanisa hilo, Tegeta Namnanga Jijini Dar es Salaam, Juzi Jumapili.
Baba Halisi
mm









































































m
m




 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana