Na Salma Amour Tanga.
Chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga kimeridhishwa na hali ya upatikanaji wa vyakula Kwa bei nafuu katika soko la mgandini na ngamiani ambapo wafanyabiashara wengi wameweza kuelewa kuwa mwezi wa ramadhan sio mwezi wa kuwapandishia wananchi bei za bidhaa kwa kiwango kikubwa kitakacho sababisha wengi wao kushindwa kununua vyakula.
Akizungumza na waandishi wa habari jumatano machi 29.3. 2023 Mara baada ya kutembelea masoko hao Mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdul Rahman ameeleza kuwa baadhi ya vyakula vimepungua bei katika kipindi hiki Cha mwezi wa ramadhan ikiwa ni Moja Mabadiliko ya uelewa juu ya wabanyabiashara hao kuwa mwezi huu si Kwa ajili ya kuwakomoa wananchi wa kuwapandishia bei za vyakula Ili kupata fedha nyingi.
"Niwapongeze wafanyabiashara wote wa soko la mgandini na ngamiani Kwa kuona umuhimu wa kuuzwa bidhaa zao Kwa bei za kawaida kama ilivyokuwa hapo awali,Kwa Sasa wafanyabiashara wengi wamekuwa waelewa kuwa mwezi wa ramadhan sio mwezi wa kuwakomoa wananchi Bali mwezi huu upo Kwa Ajili ya kuchuma mambo mema"
Katika hatua nyingine aliwataka wananchi kutowalaumu wafanyabiashara katika baadhi ya bei za vyakula kuwa juu Kwa kuwa wafanyabiashara hao wananunua kutoka Kwa wakulima Ili nao wapate faida.
.
"Wakazi wa Tanga niwaombe kuwa na uvumilivu katika baadhi ya vyakula kama ndizi za mkono wa tembo kuwa juu tumeona baadhi ya wananchi wakilalamika, lakini ukweli ni kuwa mfanyabiasha anapochukua bidhaa kutoka Kwa mkulima hawezi kununua bidhaa Kwa laki akarudisha pungufu ya hapo lakini Zaidi ni kuwa atauza Ili apate faida yake.
Kwa upande Wake Meya wa Tanga la Tanga Abdulrahman shiloow alibainisha kuwa kupitia ziara hiyo fupi ya kuangalia Hali ya bei za vyakula kwenye masoko hayo pia Kuna uhitaji wa kuiboresha miundombinu katika soko la mgandini Ili kuondoa kero ya mazingira Duni hususan katika kipindi Cha mvua.
" Halmashauri wa Jiji la Tanga Haina uwezo wa kujenga soko Hilo kwa sababu fedha nyingi zinahitajika ikiwa bajeti yake ni shilingi bilioni 17 na halmashauri yetu inakusanya shilingi bilioni 18 Kwa Mwaka lakini tumeomba Serikali kuu iweke nguvu za kutuwezesha soko Hilo kujengwa na imetuahidi kupitia fedha za mradi wa TACTIK kuwa itajenga soko la mgandini ambalo ndio soko kubwa lenye uhitaji Kwa wananchi wengi.
Nae pia katibu wa soko la mgandini shabaan Mohammed shabaan imekishukuru chama Cha mapinduzi mkoani Tanga Kwa kuwajali wakazi wa Tanga hususan katika kuangalia Changamoto mbalimbali ambazo zipo kwenye jamii.
"Niishukuru serikali ya CCM Kwa kutujali kupitia Changamoto mbalimbali tunazokumbana nazo kwenye jamii yetu, awali sikutarajia kuwa kama serikali yetu itawaza kufikiri kutujengea soko hili lakini ninaimani soko hili likipata Mabadiliko makubwa basi wafanyabiashara wote 1,600 watauza kidhaa zao katika mazingira mazuri na salama kabisa, ukweli ni kuwa kiafya sio salama Kwa wanunuzi wa bidhaa za vyakula kukuta vimewekwa chini hii pia inachangia mlipuko wa magonjwa mbalimbali Kwa walaji, na Leo nimefarijika sana kuona kuwa serikali yetu inampango madhubuti wa kutuletea maendeleo makubwa katika mkoa wetu".
Aliongeza kuwa wafanyabiashara katika masoko mbalimbali wanajali kupata baraka Kwa mungu wa kuzingatia sheria na taratibu za Imani ya dini ya kiislam Kwa kuwauzia wateja wao Kwa bei nafuu na sio kuwapandishia bei kama ilivyo zoeleka katika miaka ya nyuma hususan katika kipindi Cha mwezi wa Ramadhan.
"Watu wengi wameelimika kupitia vipindi mbalimbali vya mawaidha Kwa mashekh wetu kuwa mwezi huu mtukufu si Kwa ajili ya kutapa faida za kupitiliza ambazo hazina Baraka,Kwa kuamini kuwa lazima wateja watakuja, Kwa hili tunawashukuru sana watanyabiasha wote na mungu aendelee kuwabariki juu ya uadilifu wao".
Nae mfanyabiashara wa samaki katika soko la ngamiani Mohamed chuo ameleza kuwa mzunguko wa biashara katika soko Hilo ni mdogo kitokana na kuhamishwa kwa stendi ya pangani na horohoro kupelekwa sehemu nyingine .
*****
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Rajabu Abdul Rahman akizungumza na wafanyabiashara katika soko ngamiani kuhusu bei mbalimbali za vyakula na Changamoto zilizopo katika biashara zao
Post a Comment