Simba wameigombea Yanga kutangazwa kuwa bingwa wa Ligi Kuu baada ya kuichapa mabao 2-0 na kuendelea na mbio za ubingwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, leo.
Simba walianza kwa kasi ya ajabu na mnamo dakika ya 2 Benki Kisiki Henock Inonga aliwanyanyua mashabiki wake akifunga bao safi kwa kichwa akimalizia Krosi ya Shomari Kapombe.
Baada ya kupata bao hilo Simba waliendelea kuishambulia Yanga ambao wachezaji wake hawakuwa mchezo dakika ya 32 Kibu Denis alipigilia msumari wa pili kwa shuti kaili lililomshinda Diarra.
Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 63 na kupunguza gape la Pointi na kubaki tofauti ya alama tano huku kila timu ikibakiwa na mechi nne.
Yanga wanabaki na Pointi zao 68 ili wawe mabingwa wa Ligi msimu huu wanahitaji kushinda mechi tatu ili wafikishe Pointi 76 ambazo Simba akishinda mechi zake zote atakomea pointi 75
Sorce: Fullshangweblog.
Post a Comment