Featured

    Featured Posts

MAWAKALA WA CRDB BANK KUJIPATIA ZAWADI YA GARI ,BAJAJI NA PIKIPIKI,NCHINI.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani Tabora Naitapwaki Tukai akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mawakala wa kiume ambao wameshiriki katika semina ya kuwajengea uwezo na uelewa juu ya masuala ya fedha.

Na Odace Rwimo Nzega BENK ya CRDB hapa nchini imepanga kutoa zawadi ya Pikipiki 40,Bajaji 5 Na gari Aina ya Alphard 1 kwa Mawakala wanaofanya vizuri huduma zao kwa kipindi Cha Miaka 10.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai akiwa kwenye picha ya Pamoja na Mawakala wa Kike waliohudhuria Semina Kanda Magharibi Wilayani Nzega.

Hayo yamebainishwa na Meneja Ufanisi wa Mawakala Makao makuu Far es Salaam Goodluck Ruhago wakati akitoa semina elekezi kwa Mawakala Wilayani Nzega Mkoani Tabora

Alisema zawadi hizo ztaleta Ufanisi kwa Mawakala wengine ambao hawatabahatika kupata kwa kipindi kwa awamu hii ya Kwanza na kuwafanya kufanya vizuri ili na wao waze kupata zawadi pindi itakapo tokea fulsa Kama hiyo .

Alisema Mawakala wmekuwa nguzo mhimu ya mhimili huo wa benk.hasa maeneo ambayo Hana huduma za kibenk hivyo hutumia Mawakala hao kuwahudumia wateja waliopo mbali na benk.

Alisema ikiwa CRDB wanatimiza Miaka 10 huduma imekuwa kwa kiwango kikubwa saana hasa maeneo ya ya nchi ya Tanzania kwani wateja wengi hupata huduma Karibu yao kwakutumia Mawakala wanaopatikanamahali walipo.

Awali mkuu wa Wilaya ya Nzega Mkoani hapa Naitapwaki Tukai aliwataka Mawakala kutumia Elimu na mafunzo mbalimbali wanayoyapata kutoka kwenye benk wanazofanyia kazi kwa kutunza na kulinda Siri za wateja wao.

" Kumekuwa na malalamiko mengi ya watu kuibiwa na hiyo inatokana na baadhi ya Mawakala kutokuwa na usiri pindi wanapowahudimia wateja wao hivyo kupelekea baadhi yawateja kuibiwa fedha zao" Alisema DC Tukai.

Aliwataka Mawakala wote kuwa ujuzi wao katika kuwahudumia wateja wao na kulinda taarifa za mteja huku akiwataka kuwa na kitabu Cha kumbukumbu kwa wateja wote wanapowahudimia kuondoa utata ambao umekuwa ikijitekeza kwa baadhi ya wateja wanao wahudumia.

Katika hatua nyingine DC Tukai ameitaka Benk ya CRDB kuwapa mikpo Mawakala ili kuweza kufanya kazi zao kwa Uhakika kwani baadhi ya Mawakala wamekuwa na ufinyu wa mitaji Hali inayochangia kushindwa kuwahudumia wateja kwa wakati.

Alisema Kama Benk hiyo utaona umuhimu wa kupatia mikopo Mawakala itawasaidia kukuza mitaji yao na kutoa huduma Bora na itakayo Leta ushindani haliai wakati wanapotoa zawadi kama hizi ambazo zitaanza kutolewa mwezi June mwaka huu.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana