Featured

    Featured Posts

MWENGE WA UHURU WATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA SH. BILIONI 17.3 WILAYA YA ILALA

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog
Mwenge wa Uhuru jana ulitinga katika Wilaya ya Ilala na  kukagua kwa kishindo miradi sita yenye thamani ya jumla ya Sh. Bilioni 17.3, ukiwa katika mbio zake mkoani Dar es Salaam, ambako uliingia Mei 24, mwaka huu, ukitokea mkoa wa Pwani.

Miradi hiyo iliyokaguliwa Wilayani Ilala ni miongoni mwa jumla ya miradi 32 yenye thamani ya jumla ya sh. bilioni 23, ambayo Mwenge huo umehusishwa kuitembelea katika Wilaya zote za mkoa wa Dar es Salaam..
 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, akipokea Mwenge huo jana kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo, alitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na Barabara  katika Mtaa  Ismail Upanga Mashariki yenye urefu wa Kilomita 0.65 iliyojengwa kwa gharama ya Sh. bilioni 1.6.

Alitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa Shule ya Sekondari ya  Liwiti iliyopo Mtaa wa Liwiti unaogharimu Sh. Bilioni 3.5, Ujenzi wa tanki la maji Kata ya Zingiziwa unaogharimu Sh. Bilioni 11.2,  ujenzi wa Kituo cha  Afya Zingiziwa ( Sh. Milioni 636.5), Upandaji miti Zingiziwa (Sh.milioni 49.6) na Mradi wa Kikundi cha vijana  Kitunda wa utengenezaji vikoi na ushonaji (Sh. Milioni 180).

DC Mpogolo alimweleza Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalah Shaibu Kaimu kutoka Pemba, kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwa  fedha za mapato ya ndani ya Halmashauri na Serikali kuu.

Akizungumzia miradi hiyo, KIongozi huyo wa Mbio za Mwenye wa Uhuru Kitaifa, alipongeza viongozi wa Wilaya ya Ilala na watendaji kwa utekelezaji wa miradi hiyo vizuri.

"Katika Barabara ya Isman mwenye umekagua  nyaraka za ujenzi ziko vizuri. Pia umekagua mradi wenyewe uko vizuri japo unakasoro ndogo ya mitaro.Tunataka ndani ya siku tano irekebishwe,"alisema Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge.

Katika mradi wa Sekondari ya Ghorofa Liwiti, Kiongozi huyo alitoa maelekezo ya kutafutwa matofali yenye ubora zaidi kumalizia sehemu ya juu ili kuhakikisha jengo linakuwa imara na kudumu kwa muda mrefu.

Alisisitiza uwajibikaji, kupiga vita rushwa, matumizi ya dawa za kulevya, mapambano dhidi ya Maralia, Ukimwi, kuzingatia lishe bora na kutunza mazingira.

Mwenge huo wa Uhuru katika mkoa wa Dar es Salaam, kabla ya kungia Ilala ukitokea Kigamboni, ulikuwa umeshafika Temeke,  na leo utaendelea na mbio zake Wilayani Ungo na kesho Kinomdoni na kisha kuvuka bahari kwenda Wilaya ya Mjini Magharibi Zanzibar.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo, katika mapokezi ya Mwenge kuingia katika Wilaya ya Ilala, yaliyofanyika jana Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi, Gerezani jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalah Shaibu Kaimu kutoka Pemba,
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Halima Bulembo, katika mapokezi ya Mwenge kuingia katika Wilaya ya Ilala, yaliyofanyika jana Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi, Gerezani jijini Dar es Salaam, jana. Kushoto ni Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalah Shaibu Kaimu kutoka Pemba,
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo akizungumza jambo na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Abdalah Shaibu Kaimu kutoka Pemba wakati wa mapokezi ya Mwenge kuingia katika Wilaya ya Ilala, yaliyofanyika jana Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi, Gerezani jijini Dar es Salaam, jana.
DC Mpogolo akizungumza katika mapokezi ya Mwenge huo wa Uhuru.
Mtaalam akionyesha michoro ya mradi wa barabara ulitekelezwa
Mradi wa ujenzi shule ya Sekondari Liwiti.
Mradi wa Maji Zingiziwa.
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana