Featured

    Featured Posts

RAIS SAMIA AMTEUA KIHONGOZI KUWA DC, AMPANDISHA MTANDA KUTOKA DC KUWA RC, AWAPANGUA MAKONGORO NYERERE NA SENDIGA, LEO

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Dar es Salaam
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Kenani Kihongozi kutoka Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo, huku akimpandisha Saidi Mtanda kutoka Mkuu Wilaya ya Urambo kuwa Mkuu wa mkoa wa Mara.

Taarifa iliyotolewa leo na Ikulu, Chamwino Jijini Dodoma imesema, Mtanda amepandishwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Mara kuchukua nafasi ya Meja Jenerali Suleiman Mzee ambaye amepangiwa majukumu mengine na Kihongozi akichukua nafasi iliyoachwa na Mtanda.

Kulingana na Taarifa hiyo Quuen Sendiga amehamishwa mkoa wa Manyara alikokuwa Charles Makongoro Nyerere, ambaye naye mehamishiwa mkoa wa Rukwa alikotoka Sendiga.

Taarifa imesema Mabadiliko, Uhamisho na Uteuzi huo unaanza mara moja na uapisho wa Mkuu mpya wa mkoa utafanyika kesho Mei 34, 2023, saa 10 jioni Ikulu, Chamwino , Dodoma.

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa kazini
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana