Featured

    Featured Posts

TAZAMA MAMIA WALIVYOMIMINIKA KWA BABA HALISI KUPOKEA UPONYAJI ALIOUACHILIA KWA JINA LA MUNGU MWENYEWE

Tegeta Namanga, Dar es Salaam

Jumapili iliypita ya Mei 14, 2023, (19 Zivu 1 Majitra Halisi), mamia ya watu walimiminika kushiriki Ibada Maalum ya Uponyaji iliyofanyika Kao Kuu la Kanisa Halisi la Mungu Baba, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam, ikiendeshwa na Kiongozi Mkuu wa Kanisa hilo ndani na nje ya Tanzania, Baba Halisi.

Kabla ya kuanza kuachilia Uponyaji huo, Baba Halisi aliweka wazi kwamba, uponyaji huo ataufanya kwa Mamlaka ya Mungu Baba mwenyewe tofauti na ambavyo wengi wamekuwa wakifanya uponyaji huo kwa Jina la Mwana (Yesu).

"Hapa nitafanya uponyaji kwa Mamlaka ya aliyetuumba, hamtasikia namtaja Yesu, siyo kwamba namdharau, hapana, maana mimi pia nimewahi kumhubiri sana, lakini sasa Yesu alisharejesha mamlaka yote kwa Mungu Baba, hivyo siyo wakati wake tena", akasema Baba Halisi huku akifafanua kwa kina kupitia kitabu.

Baada ya kueleza ufafanuzi huo, Baba Halisi alianza kuachilia uponyaji kwa kuanza yeye kula kipande cha ndizi, kisha akaanza kumpa mmoja bada ya mwingine tukio ambalo lilidumu kwa zaidi ya saa moja.

Baadaye Baba Halisi aliwaomba wale wote waliopokea uponyaji huo, kwenda kupima magonjwa wanayodhani kuwa walikuwa nayo ili jumapili ijayo wapeleke mraejesho.

"Jumapili nilikuwa niende Dodoma, lakini kwa sherehe hii ya uponyaji tuliyofanya sitaenda, naomba wale wote waliokuwa wanasumbuliwa na magojwa waende kupima, halafu Jumapili walete vyeti hapa, ili tupate mrejesho", akasema Baba Halisi.

Tafadhali tazama Baba Halisi akiachilia Uponyaji huo uliofanyika Kao Kuu la Kanisa Halisi, Tegeta Namanga jijini Dar es Salaam. BOFYA HAPO👇


 
author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana