Featured

    Featured Posts

ZIARA YA RAIS MSTAAFU KIKWETE KOREA KUSINI

 Rais Mstaafu Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, ambaye ni  Mwenyekiti wa Bodi ya  Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education) - GPE) yuko Seoul, Korea Kusini kwa ajili ya kukutana na viongozi wa Serikali na Mashirika Mbalimbali ya Korea Kusini kwa ajili ya kujadili mikakati ya kuendelea kuboresha elimu katika nchi zinazoendelea. GPE ambayo ilianzishwa na nchi za G7 miaka 20 iliyopita, imeendelea kupigania elimu kwa ajili ya mtoto wa kike na wa kiume kwa kuomba kuungwa mkono na nchi na taasisi zinazoweza kuchangia katika elimu duniani.


Mheshimiwa Kikwete ameambatana na Bw. Charles Noth, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo yenye makazi yake Washington DC, Marekani. 


Akiwa Seoul, amekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Balozi Park Yongmin, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini. 


Aidha, amekutana na Bw. Lee Yunyoung, Kaimu Rais wa Shirika la Serikali ya Korea la Maendeleo Kimataifa (KOICA).


Pia amekutana na Mheshimiwa Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Ban Ki-moon. 


Kesho Mheshimiwa Rais Kikwete anatarajiwa kuzungumza na Wabunge wa Korea Kusini na kufanya mazungumzo na Mhe. Ju-ho Lee, Naibu Waziri Mkuu wa Korea Kusini ambaye pia ni Waziri wa Elimu wa nchi hiyo.


Mheshimiwa Rais Mstaafu Kikwete pia ametembelea Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijini Seoul, Korea Kusini na kuzungumza na wafanyakazi. Akiwa na mwenyeji wake Balozi Togolani Mavura, amewahimiza kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na kuunga mkono kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana