Featured

    Featured Posts

MJEMA AWATAKA VIJANA KUWA CHACHU YA MABADILIKO CHANYA NCHINI

 



📍Dar es Salaam

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Ndg. Sophia Edward Mjema  Leo Tarehe 11 Juni 2023, ameshiriki kama mgeni rasmi kwenye mahafali ya seneti ya Vyuo na Vyuo vikuu Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Ubungo Plaza Jijini Dar es salaam. 


 Mama Mjema amewasisitiza Vijana wa vyuo na vyuo vikuu kuwa chachu ya mabadiliko  chanya Nchini na kuendelea kukipigania  na kukilinda Chama na Viongozi wake Hususan Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan.

 

 _" *Hatutokubali , Hatuko Tayari Kuona Mwenyekiti   Wetu Anachezewa Chezewa  , Mwenyekiti wetu ni mtu imara na makini aachwe afanye kazi ya kuleta maendeleo Nchini".*_ 


Mahafali ya seneti ya mkoa wa dar es salaam , yalihudhuriwa na takribani wanafunzi 500, kutoka matawi ya vyuo 43 , Jijini Dar es salaam. 


#Kaziiendelee

 

author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana