Featured

    Featured Posts

ZIARA YA MNEC HAMOUD WILAYA YA KIBAHA JIJINI, ASEMA CCM INATAKA VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI SIYO VYA 'CHAWA'

Na Bashir Nkoromo, CCM Blog, Pwani
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Makao Makuu kimesema hakivitambui vikundi vinavyojiita 'Chawa' na kwamba vikundi hivyo havina baraka ya Chama, hivyo wale wote wanaokipenda chama waunde vikundi vyenye faida vya ujasiriamali.

Hayo yamesemwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abou Jumaa, akizungumza na Viongozi na Wanachama wa CCM katika mkutano uliofanyika Mlandizi, akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Chama wilaya ya Kibaha Vijijini mkoa wa Pwani, jana.

" Kuna jambo moja linaendeleaendelea la Chawa, Chawa, likiihusisha CCM, na uziri baadhi ya viongozi wa Chama mpo hapa, hili neno linatambatambaa sana, sasa CCM Makao makao makuu tunasema hilo Chawa cahawa halina baraka za CCM.

Hivi vikundi cha chawa unaweza ukaanzisha iwe Chawa, nyuki, panzi au mdudu yeyote hatukatai, lakini siyo kwa faida ya CCM, cha msingi ni kuunda vikundi vyenye faida vya ujasiriamali", alisema Mjumbe huyo wa NEC. na kuongeza kuwa ametoa tamko hilo kwa nafasi yake ya Mjumbe wa NEC kwa kuwa ni maelekezo ndani ya Chama ngazi ya taifa.

Akizungumzia Uhai wa Chama Mjumbe huyo wa NEC, aliwataka viongozi na wanachama wa CCM  njia ya kwanza ya kuimarisha uhai wa CCM na Jumuiya zake ni kuhakikisha wanakuwepo wanachama hai na kinachofuata ni mshikamano wa viongozi na wanachama kufanya kazi kwa umoja na mshikamano wa dhati.

Alisema, kuwepo kwa wanachama hai na mshikamano ndiyo njia pekee ya uhakika itakayoweza kukifanya Chama kishinde katika Uchaguzi unaokuja wa Serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025, na kusisitiza kuwa hayo ni lazima yafanyike kwa kuwa lazima CCM ishinde katika chaguzi hizo.

Mjumbe huyo wa NEC alisema, tayari Mwenyekiti wa CCM Rais Samia ameshanyoosha njia ya kuifanya CCM ishide, kwa kuwa ndani ya miaka miwili ya Uongozi wake, Serikali imetekeleza miradi mingi ya maendeleo, na mingine ipo katika hatua za utekelezwaji.

Katika ziara hiyo Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mjumbe huyo wa NEC alikagua utekelezaji wa ilani ya CCM kwa utembelea miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Ofisi za CCM Matawi ya Saidi Domo na Mkwani, Zahanati ya Vikuruti, Mradi wa Zahanati Ruvu Maji na eneo la Viwanda.

Baada ya kutoka Kibaya Vijijini mkoa wa Pwani jana, leo Mjumbe huyo wa NEC anaendelea na ziara hyo ya Kitaiafa katika mkoa wa Dar es Salaam.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abuu Jumaa akivishwa skafu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mlandizi mkoa wa Pwani, kufanya ziara ya siku moja katika Wilaya hiyo, jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abuu Jumaa akiongozwa na Katibu Msaidizi Makao Makuu Jumuiya ya Wazazi Oganaizeseni Makao Makuu Ndugu Fadhili Mrami, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mlandizi mkoa wa Pwani, kufanya ziara ya siku moja katika Wilaya hiyo, jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abuu Jumaa akisaalimiaa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkali Kanusu baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mlandizi mkoa wa Pwani, kufanya ziara ya siku moja katika Wilaya hiyo, jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abuu Jumaa akisani Kitabu cha wageni baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mlandizi mkoa wa Pwani, kufanya ziara ya siku moja katika Wilaya hiyo, jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abuu Jumaa akipokea taarifa ya Chama kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, baada ya mapokezi, baada ya kuwasili Ofisi ya CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini, Mlandizi mkoa wa Pwani, kufanya ziara ya siku moja katika Wilaya hiyo, jana.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamoud Abuu Jumaa akionyesha taarifa hiyo ya Chama bada ya kukabidhiwa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Kibaha Vijijini akisoma muhtasari wa taarifa ya Jumuiya hiyo.
 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Morogoro Rose Rwakatare akisalimia baada ya kutambulishwa, alifika kuunga mkono ziara ya M-NEC Hamoud katika Wilaya ya Kibaha Vijijini mkoa wa Pwani.
Katibu Msaidizi Jumuiya ya Wazazi Makao Mkuu, Ndugu Fadhili Mrami akisalimia bada ya kutambulishwa.
 
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha Vijijini akimkaribisha M-NEC Hamoud kuzungumza.
MNEC Hamoud akizungumza. 
M-NEC Hamound akiongozwa kwenda kuzindua ujenzi wa Ofisi ya CCM la Saidi Domo.
M-NEC Hamound akizindua ujenzi wa Ofisi ya CCM la Saidi Domo.
M-NEC Hamound akiongozwa kwenda kuzindua ujenzi wa Ofisi ya CCM la Mkwajuni.
M-NEC Hamound akizungungumza baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Vikuruti.
M-NEC Hamound akipandisha bendera ya CCM baada ya kuzindua Shina la Wakereketwa la Jumuiya ya Wazzi Amani.
M-NEC Hamound akizungumza na Wanachama wa CCM na Jumuiya zake baada kuzindua Shina la Wakereketwa la Jumuiya ya Wazazi Amani.


M-NEC Hamound akipewa maelezo ya Ujenzi wa Kituo cha Polisi alipotembelea mradi wa eneo la Viwanda Kamaka.
M-NEC Hamound akipewa maelezo kuhusu maendeleo ya Zahanati ya Ruvu-Maji alipoitembelea.
M-NEC Hamound akiwa amewasili meza kuu kwenye Mkutano wa mwishoni mwa ziara yake uliofanyika Mlandizi.
Wanachama wa CCM na Juuiya zake wakiwa wamefurika ukumbini baada ya M-NEC Hamound kuwasili kuzungumza nao.
M-NEC Hamound akizungumza katika mkutano huo.
M-NEC Hamound akizungumza katika mkutano huo.
Shamrashamra zikitawala ukumbini kumshangilia MNEC Hamound. 
MNEC Hamoud akikabidhi maelfu ya kadi za Jumuiya ya Wazazi kwa ajili ya kuongeza wanachama.
MNEC Hamoud akiwa na baadhi ya viongozi wa meza kuu wakati akisubiri kupewa zawadi na makundi mbalimbali ya CCM na Jumuiya zake


 
 

 

 
 
 

 
 


author

Author Name

Author Description!

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

www.CodeNirvana.in

Magazeti Ya Leo

Copyright © Magazeti ya Leo, Habari Leo Tanzania, Mwananchi, Michuzi, mwanaspoti, nipashe, Udaku | Designed By Code Nirvana